DR. ULIMBOKA AREJEA NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI ALIKUKUWA KWA AJILI YA MATIBABU

on Sunday, August 12, 2012 - No comments:

Hivi ndivyo ilivyokuwa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere DSM leo mchana.

Hivi leo majira ya saa saba Dr. Ulimboka aliyekuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. Hali hiyo ilimkuta baada ya kutekwa na watu wasiojulikana na kumpiga na kumtesa kisha kumtelekeza njiani Pande Pwani.

Baada ya kurejea Dr. Ulimboka alipokewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wenye mapenzi mema na wanaharakati.

Dr. Ulimboka alipewa nafasi ya kuzungumza machache kwa watanzania na kitu cha kwanza alichokiongea ni kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na watanzania wote kwa kuwa pamoja nae kwa kila jambo na hasa katika kipindi chote cha matibabu kwake.

Pia Dr. alitoa shukrani zake za zati kwa Mwenyezi Mungu kwani ndiye aliyemuwezesha hata kuifikia siku hii na kuwa anafuraha kubwa kwa hatua yake ya kiafya aliyofikia kwani alisema anawahakikishia watanzania kuwa amepona na yuko fiti kabisa kwa kufanya lolote lile.

Na bila kusahau alitoa shukrani zake kwa madaktari wenzake kwa kuwa wamekuwa pamoja nae katika kila jambo.
BE BEST IS WISHING YOU ALL THE BEST IN YOUR HEALTH.
DR. ULIMOKA KABLA YA KUTEKWA ALIPOKUWA AKIONGEA KITU KATIKA MOJA YA MIKUTANO

DR. ULIMBOKA ALIPOOKOTWA BAADA YA KUTEKWA

HAPA NI DR. ULIMBOKA ALIPOKUWA WODINI

DR. ULIMBOKA AMERUDI,
JE NI NINI HATIMA YA ALIYEFANYA MAASI HAYO? NA
JE NINI TAMKO LA MAHAKAMA KUHUSIANA NA SUALA LA UTEKAJI WA DR. ULIMBOKA?.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends