DIAMOND PLATNUMZ ASHARE WIMBO WA ALI KIBA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK

on Monday, June 29, 2015 - No comments:

Kama unavyoiona hapo juu hiyo ilikuwa ni siku za nyuma zaidi ya miaka miwili iliyopita, hakukuwa na tofauti kati ya wasanii hawa waili Diamond na Ali Kiba na kama zilikuwepo basi zilikuwa ni za chinichini kiasi hata mashabiki hawakuweza kuzijua na isitoshe kwa wakati huo hakukuwa na ushindani mkubwa kati yao kitu amacho ni tofauti na sasa kila mmoja anataka kuwa juu ya mwenzake na kuonekana yeye ni bora zaidi kuliko mwenzake.
Hadi sasa bado imekuwa ni utata mkubwa juu ya wasanii hawa vinara kabisa hapa nchini na kusababisha mgawanyiko mkubwa sana wa mashabiki kitu kilichopelekea kuzaliwa kwa timu mbalimbali za ushabiki wa mziki wa Bongofleva ambazo zimekuwa zikizidi kushika kasi huku kila timu ikijitahidi kuuandika vibaya upande mwingine ilimradi tu kufanya timu yake na mtu wake aonekane yuko juu zaidi ya mwenzake.
Wadau na wasanii mbalimbali wameonekana kukerwa sana na timu hizo kwani zinapelekea kuwaingiza na wasanii na wadau wengine katika ugomvi huo, mfano Davido kutoka Nigeria alikereka na Timu Kiba ilipoonekana kujaza maneno ya kumdhihaki msanii Diamond katika ukurasa wake katika kinyang'anyiro cha tuzo za MTVMAMA 2015. Pia wasanii Aika na Nahreal Mkono kutoka kundi la Navy Kenzo wameliongelea suala hilo katika upande hasi masaa machache yaliyopita katika kituo cha luninga cha EATV.
MUNGU AWAJAALIE WASANII HAWA WAWILI WAWEZE KUKETI CHINI NA KUZIMALIZA TOFAUTI ZAO KWANI NAAMINI NI WAAMINI SAFI WA DINI NA DINI SIKU ZOTE HUIMIZA UPENDO.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends