WANANCHI WA MTWARA, TUMEWALETEA CHAMA KIPYA, MH. ZITTO KABWE

on Thursday, June 25, 2015 - No comments:

Wananchi wa Mtwara tumewaletea chama kipya. Chama ambacho kimeundwa kwa misingi imara ya kurejesha uzalendo, Utu na Undugu. Chama kinachokuja kuondoa siasa za ujanja ujanja na kujenga siasa za hoja. 
Mtwara na mikoa ya kusini mmekuwa ngome ya Ulinzi wa nchi yetu kwa muda mrefu sana dhidi ya maadui wareno. Kutokana na hali hiyo mikoa hii imekuwa nyuma sana kimaendeleo. Sasa kuna Neema inaonekana katika mikoa hii na ni wajibu wa viongozi wa sasa wa kisiasa kuhakikisha utajiri uliopatikana katika mikoa hii inatumika kwa maendeleo ya Kusini na Tanzania kwa ujumla.

ACT Wazalendo inataka kubadili siasa zetu ili kuwa na siasa za masuala na kuondokana na siasa za kutukanana, kuzushiana na kusema uwongo. Tunataka siasa za majawabu ya kero za wananchi. Kwa Mtwara na mikoa yote ya kusini tunataka kuwa nanyi katika changamoto kuu 2; kilimo na Biashara ya Korosho na utajiri wa mafuta na gesi Asilia. Leo hapa masasi tutaongelea Korosho
Korosho 
Chama chetu kinajua changamoto katika sekta ndogo ya zao la Korosho na tuna dhamira ya dhati ya kumaliza kabisa changamoto hizo. Wakulima wa Korosho hawafaidiki kabisa na kilimo na kila mwaka wanaendelea kudidimia kwenye dimbwi la umasikini. 
Mwaka 2005 wakati Mkapa anaondoka madarakani bei ya Korosho kwa kilo ilikuwa tshs 900 na bei ya dawa ya sulphur ilikuwa tshs 7000 kwa lita 20. Mwaka 2015, miaka 10 baadaye kilo ya korosho inauzwa kwa tshs 1000. Hata hivyo dawa ya sulphur imeongezeka bei maradufu mpaka tshs 15,000 kwa bei ya Serikali na tshs 45,000 kwa bei ya kulangua. 
Vyama vya ushirika vinanunua korosho kwa mkopo na hivyo kuvuruga kabisa mipango ya wananchi kujiletea maendeleo yao binafsi. 
Kwa mfumo huu Serikali ya chama cha mapinduzi imefukarisha wananchi wa Kusini kwa kuweka sera mbaya kuhusu Korosho. Mfumo wa stakabadhi ghalani bado haumsaidii mkulima bali unasaidia watu wa kadi ambao ndio ilikuwa lengo la kuwaondoa. 
ACT Wazalendo inataka kuvunja vunja mfumo huu wa middle men katika soko la Korosho kwa kuwawezesha wakulima kupitia mfumo wa hifadhi ya jamii. Kwa kuwa Korosho inauzwa kwenye soko la Dunia kwa dola ya marekani hivyo hivyo wakulima walipwe kwa dola ya marekani ili wapate malipo halisi. Hili sio jambo geni kwani tayari mfumo huu unatumika kwenye Tumbaku. 
Hifadhi ya jamii kwa wakulima itawezesha vyama vya ushirika kukopa kutoka kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii na kununua Korosho kwa wakulima bila kukopa. Kupitia Hifadhi ya jamii pia kila chama cha msingi kitaweza kubangua Korosho zake na kuziuza sokoni zikiwa zimeongezewa thamani. Kwa njia hii ndio wakulima watafaidi kilimo chao. 
Korosho inachangia mabilioni ya fedha kwenye mapato ya fedha za kigeni. Mwaka 2014 Korosho iliingiza dola za kimarekani 222 milioni ikichukua nafasi ya pili baada ya tumbaku iliyoingiza dola 315 milioni. Katika fedha hizi mkulima alipata 35% tu ya fedha yote hii takribani tshs 450 bilioni. Iwapo Korosho hii ingeuzwa ikiwa imeongezewa thamani tungepata mapato zaidi ya dola 150 milioni. 
ACT Wazalendo haina malengo ya kutaifisha Mali ya mtu bali tunataka kurekebisha makosa ya ubinafsishaji holela uliofanyika na kuuza viwanda vya kubangua Korosho. Kwa mujibu wa Azimio la Tabora itakuwa ni marufuku kwa Tanzania kuuza malighafi nje ya nchi. Korosho itakuwa zao la kwanza kutekeleza sera hiyo.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends