TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU, ARSENAL WENGER AKANA TAARIFA ZA KUMSAJILI BENZEMA NA NYINGINE ZIKO HAPA

on Monday, August 3, 2015 - No comments:

 
Menenja wa Arsenal Arsene Wenger ametupilia mbali taarifa zinazomhusisha na kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 27 (Evening Standard), hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la AS, Wenger ametenga pauni milioni 45.6 kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. 
Arsenal wamewazidi Manchester United katika kumsajili kipa mwenye umri wa miaka 15 kutoka Benfica Joao Virginia (Metro), meneja wa Wolfsburg Dieter Hecking anaamini kiungo Kevin de Bryne, 24, hatokubali kwenda Manchester City (Manchester Evening News), lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amesema ni vigumu kukataa kuhamia Etihad (Sun), Manchester City wanakabiliwa na ushindani mkali kubakia na kiungo Marcos Lopes,19, huku Marseille, Monaco na Lyon wakimtaka mchezaji huyo kutoka Ureno (Daily Mail), meneja wa Sunderland Dick Advocaat ana matumaini ya kumsajili kiungo wa Rubin Kazan Yann M'Vila, 25 na kiungo wa QPR Leroy Fer (Daily Star), Manchester United wamempa winga wao Ashley Young mkataba wa miaka mitatu. Mchezaji huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake (Daily Star), beki wa Manchester United Rafael Da Silva anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 2.1 kwenda Lyon (Times), Tottenham wapo tayari kuingia hasara ya pauni milioni 15, kwa kumuuza mshambuliaji wao Roberto Soldado baada ya kuanza mazungumzo na Villareal kwa pauni milioni 11 (Daily Mirror), Liverpool wanatazama uwezekano wa kutoa pauni milioni 14.9 kumsajili winga wa Real Madrid Denis Cheryshev 24 (Daily Telegraph), meneja wa Everton Roberto Martinez ana uhakika kuwa atamshikilia beki wake wa kati John Stones, 21 ambaye anawindwa na Chelsea (Liverpool Echo), Juventus wanataka kumnyatia Javier Mascherano kuziba pengo la kiungo Sami Khedira ambaye ni majeruhi (Tuttosport), Louis van Gaal amempa makataa Ed Woodward kuhakikisha anakamilisha usajili wa kipa Jasper Cillisen na David De Gea kuuzwa kabla ya Jumamosi (Daily Mirror).

Tagged as: ,
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends