TIGO WAZINDUA UDHAMINI WA MBIO ZA NUSU MARATHON MJINI MOSHI

on Friday, January 22, 2016 - No comments:

Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

 Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, akifafanua jambo   kwa waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Tigo kwa mbio za Nusu Marathon mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga(watatu kushoto, ).akizindua mbio za Kilimanjaro Marathon kwa upande wa Moshi. Wengine ni wadhamini wakuu wa mbio hizo kutoka kushoto, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania-Kilimanjaro na Tanga, Richard Temba, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Listone Metacha na Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Caroline Kakwezi.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

Wageni waalikwa ambao  ni wadhamini wa Kili Marathon wakifurahia jambo baada ya Mkuu wa wilaya Mh Novatus Makunga kuzindua mbio za Kili Marathon kwa upande wa Moshi ambapo zitafanyika hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

Mbio za Nusu Marathon 2016 zimezinduliwa jana mjini Moshi, huku ikiwa imebaki mwezi moja kabla za mbio hizo kufanyika.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari alisema mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.
“Tumeonelea ni vizuri kuzindua mbio hizi rasmi hapa Moshi  ambako zitafanyika ili kuashiria kuwa mambo yamekamilika,” alisema.
“Tigo imeingia mwaka wake wa 2 kama mdhamini wa mbio za kilomita 21.2 hizi. Kwa mujibu wa Meneja huyo, wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Kilimanjaro beer 45, Gapco kwa km 10 viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt kwa km 5.
Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair na Keys Hotel.
Alisema Tigo imewekeza zaidi ya Sh Millioni 200 katika mashindano hayo na kuwa hapo badaye watatangazo mchanganuo mzima wa zawadi zitakazotolewa.
Alitoa shukrani za pekee kwa mkoa wa Kilimanjaro na chuo kikuu cha Ushirika MOshi (MoCu), zamani kikiitwa MUCCoBS kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Akizindua mbio hizo mjini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makung, aliwapongeza Kilimanjaro Premium Larger,Tigo wadhamini wengine na wandaaji kwa kujielekeza vyema  kila mwaka, akiongeza kuwa mashindanoyametokea kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kimichezo ndani na nje ya nchi.
“Mashindano haya pia yamekwenda mbali zaidi katika kukuza utalii, kwani wanariadha wa kimataifa na wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hiyo kufaidisha uchumi wan chi,” alisema Makunga.
Makunga aliawataka wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanajiandaa vyema ili watwae zawadi nyingi zaidi kwa kadiri zilivyopangwa kwa kila mbio. Aliongeza kwamba wizara yake inaunga mkono kabisa ubunifu kama huo na kuzitaka kampuni nyingine kufuata nyayo hizo kwa kudhamini mashindano hayo kila mwaka.

Aliwapongeza wandaaji, Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa Executive Solutions, Chama cha Riadha Tanzania (RT) na wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha siku zote kwamba tukio hili linafikiwa .
“Mbio hizi zimeleta mwamko mpya katika riadha hapa nchini kwa kuwapa fursa vijana wetu wanaochipukia kuweza kujipima na wanariadha mashuhuri kimataifa. Changamoto hii imekuwa na faida kubwa,ambapo vijana wetu wameweza kutambua uwezo wao na kuweza kujiamini  zaidi wanapokwenda kushiriki mashindano mbalimabli kwenye nchi za kigeni,” alisema.

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, alisema kwamba kampuni yake imefurahishwa kupata fursa ya kudhamini mbio za nusu marathoni kwa kilimota 21 kwa mwaka wa pili mfululizo.
“Natoa rai kwa washiriki wajiandae vizuri ili safari hiituweze kunyakua mataji mengi,” alisema Kinabo.

Meneja Masoko wa Gapco Tanzania, Caroline Kakwezi, ambaye kampuni yake inadhamini mbio za kilomita 10 kwa wanaotumia viti vya magurudumu na wale wanaonyonga baiskeli kwa mikono ambazo wanazidhamini, alisema zimekua na mvuto mkubwa na ushindani mkubwa pia na kwamba katika mwaka wao wa tano katika udhamini wameshuhudia mbio hizo zikikua.

“Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono, safari hii tutatoa usafiri, malazi na chakura kwa washiriki wote kutoka Dar es Salaam katika mbio hizi za walemavu na yote haya hayawezekani bila ushirikiano tunaoupata kutoka kwa wateja wetu”alisema.


Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends