fastjet yashinda kwenye Tuzo Za Usafiri Duniani

on Thursday, April 14, 2016 - No comments:





TAARIFA KWA NYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam – 11 April 2016 –fastjet, shirika la  ndege la gharama nafuu barani Afrika imeshinda Tuzo ya Shirika la Ndege Linaloongoza Afrika kwa Gharama Nafuu kwenye Tuzo ya  23 ya Mwaka  ya  Usafiri Duniani iliyotolewa Zanzibar, Tanzania  Aprili 9, 2016.

Tuzo ya Usafiri ambayo inatambulika  duniani  imepangwa kwa kutambua, kutuza na kusherehekea  mafanikio kwenye  sekta zote muhimu  za usafirishaji  wa kwenye sekta ya utalii.

 Tuzo ya Shirika la Ndege Linaloongoza kwa Gharama Nafuu  ambayo hutolewa kwa wataalamu wa  usafiri na utalii pamoja an watumiaji duniani kote  inatokana na kutambua  huduma za fastjet za kufanya watu wamuumudu usafiri wa anga, usalama na kuaminika  kwenye mtandao yote barani Afrika.

“Kutambuliwa na kupata tuzo hii sio tu kunaonesha  kujituma kwa ufanisi kwenye usafiri wa anga, lakini kunaonesha matokeo ya juhudi zetu  tunazojaribu kulifanyia bara la Afrika,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania,  John Corse na kuongeza, “tunajivunia sana  kupokea kutambuliwa huko na sekta hii kubwa  na fastjet itaendelea  kuufanya usafiri wa anga  kuwa wa gharama za chini ambazo watu wengi watazimudu  barani Afrika.”

Shirika hilo la ndege la bei nafuu  lilizinduliwa  Novemba 2012 na linafanya safari kadhaa za ndani ya Tanzania  kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya, Mwanza na Kilimanjaro. Kukua kwa mtandao wa fastjet  pia kunatoa huduma  kwa njia ya kutoka Dar es Salaam na Zanzibar na kwenye vituo vya kimataifa  kama vile Johannesburg, Harare, Victoria falls, Entebbe, Nairobi na Lusaka.

Fastjet inatarajia  abiria wake wengi kwenye njia hizo inakotoa huduma  kuwa ndio wanasafiri kwa mara ya kwanza kwa kutumia ndege  kutokana na sababu ya kukwazwa na tozo za nauli ya juu  ambazo awali  hawakumudu kulipa kwa ajili ya usafiri huo.

Huduma hii ya nauli nafuu imeungwa mkono kwenye utafiti uliofanywa na shirika hilo hivi karibuni, unaoonesha kuwa asilimia 40 ya abiria  kwenye njia zote walikuwa ndio mara yao ya kwanza kusafiri kiumudu kusafiri kwa ndege  kwa mara ya kwanza  hivyo pongezi ziende kwa gharama nafuu za fastjet.

Jambo jingine ambalo linapatikana kwenye  njia inamopita fastjet ni kuboreshwa kwa mbadala wa mzigo  ambako kunajulikana kama ‘freighty’ kunakoruhusu abiria  kusafirisha  hadi kilo 80 zilizofungwa kwenye mabegi kwa  gharama ya shillingi 88,000. Mbadala huo wa kusafirisha mizigo kimsingi umekuwa ni maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na fastjet  kwenda kununua bidhaa za jumla kimataifa na kuzisafirisha kwa ajili ya kuziuza  kwenye masoko ya  nyumbani mwao.

 Tuzo hii inaongeza  idadi ya tuzo  ambazo fastjet imeshazipata  zikiwemo kushinda Tuzo ya Ubunifu kwenye Usafiri kwenye utoaji wa nane wa tuzo hiyo mwaka 2015, na hali kadhalika  kutangazwa kuwa  shirika la ghama  nafuu barani Afrika katika kulinganishwa  mengine kwenye usafiri wa anga kupitia mtandao wa safiri  WhichAirline.com in 2016.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends