Mke wa aliyekuwa Raisi wa Kenya Mh. Mwai Kibaki afariki dunia

on Tuesday, April 26, 2016 - No comments:Na, Kaozat.
Mke wa aliyekuwa Raisi wa awamu iliyopita aliyemaliza muda wake nchini Kenya Mh. Mwai Kibaki amefariki dunia nchini Uingereza ambako alikuwa huko kwa ajili ya kupata matibabu katika hospitali ya Bupa Cromwell. Taarifa hiyo imetolewa na Raisi wa sasa wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta na pia imetangazwa na Televisheni ya KTN ya nchini Kenya.

Marehemu Lucy Kibaki (76) alizaliwa mwaka huko Mukurwe-Ini, Nyeri na kuolewa na Kibaki mnamo mwaka 1962. Katika maisha yao ya ndoa walifanikiwa kupata watoto wanne (4) Judy Kibaki, Jimmy Kibaki, Tony Kibaki, David Kibaki.

Umaarufu mkubwa aliojizolea Bi Lucy ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuwasaidia watu wenye mahitaji muhimu katika jamii kama walemavu na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMEN.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends