Nini sababu inayokufanya uoe sasa? Kosea njia utaelekezwa, lakini sio kuoa.

on Friday, April 8, 2016 - No comments:


  • Usioe kwa sababu umechoka kula kwa mama lishe>>Mke sio mpishi kama umechoka kula kwa mama lishe jifunze kupika.
  • Usioe kwa sababu umechoka kufua na kupika >>Mke sio housemaid, kama umechoka kufua ajiri mtu akufulie.
  • Usioe kwa sababu rafiki zako wote wameoa >>Mke sio mashindano maana hataishi na marafiki zako wala sio zawadi kwa wazazi wako bali wewe ndiwe utakayeishi naye.
  • Usioe kwa sababu unataka kufungua kanisa sasa unatafuta mama mchungaji
  • Usioe kwa sababu wazazi wanakulazimisha maana dada zako wote wameshaolewa.
  • Usioe kwa sababu mpenzi au mchumba amepata mimba yako.
  • Usioe kwa sababu unataka kumuonyesha msichana aliyekuacha kuwa bado upo juu.
  • Usioe kwa sababu unamhurumia msichana uliyenaye ukimuacha atachanganyikiwa.
  • Usioe kwa sababu wazazi wako wanampenda na kumkubali msichana huyo.
  • Kuliko kumuoa msichana kwa kumhurumia na si kumpenda itapelekea kuteseka moyoni maisha yenu yote ni afadhali umwambie ukweli kungali mapema
  • 11: Kuoa ili kujionyesha kuwa ume-move on baada ya kuachwa ni kujikomoa mwenyewe.
Oa ukiwa na uhakika kuwa huyo ndiye chaguo lako pekee na upo tayari kuishi naye katika hali zote, ndio mpango wa Mungu katika maisha yako na ndiye unayempenda kwa moyo wako wote.

By Daniel Burton Mwaseba

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends