Simulizi: Chozi la furaha

on Sunday, May 8, 2016 - No comments:

MTUNZI; Moringe Jonas Mhagama
MAWASILIANO; jonasymoringe@gmail.com
Nilishuka garini nikiwa na furaha,hii baada ya kutoka likizo baada ya miezi sita ya kukaa chuoni.Mtu wa kwanza kumuoana alikuwa ni mama yangu ambaye alikuwa amemshika mkono mdogo wangu ambaye alikuwa darasa la kwanza.Nilimkumbatia mamangu huku nikiwa siamini kwani safari ya kutoka moshi hadi Ludewa ni safari ichoshayo na yenye misukosuko mingi sana.Baada ya kumwachia mama nilimbeba mdogo wangu ambaye baada ya kunisalimia aliniuliza kama nitamsimulia hadithi tena nilimjibu kuwa atasimuliwa na mama kwani nilibeba kitabu cha hadithi.Tulitoka huku nikimuuliza mama juu ya jamaa zangu niliokuwa ni lazima niwaulizie kila nifikapo.Tulifika nyumbani ambapo baada ya kusalimiana na babu na bibi nioga wakati huo mama alikuwa ananiandalia chakula, baada ya kula chakula ambacho nilikiona kitamu sana asikuambie mtu chakula cha mama kilivyokitamu we acha tu(mola wapokee waliotangulia mbele ya haki).
Baada ya kula chakula kile ambacho nilionekana kukitamani kwa muda mrefu ,ugali wa mhogo na
samaki wa kuchomwa ,nilikaa na mama yangu tukiongea hili na lile kwani alitaka kujua mengi kuhusu safari yangu na maendeleo ya shule.Nikweli alijivunia kwani nilikuwa ni mwanaye wa kwanza wa kiume na pekee aliyefikia Chuo kikuu na mwanaye wa mwisho alikuwa darasa la kwanza.
Nyumba ilikuwa na ukimya sana baada ya yote yaliyotokea kwenye SIRI YENYE MATESO kiukweli hatukuwa na marafiki wengi wa familia kama pale kale, mama alitumia muda huo kunieleza yaliyotokea nilivyokuwa shuleni na alinitaka nikazane na nijitume kwani aliamini hakuwa  na ndugu mwingine zaidi ya sisi wanawe kwani babu alikuwa ni mzee sana na muda wowote tungemzika kwani tayari alifikisha miaka tisini na nane.Nilijikuta natokwa na machozi kwani mdogo wangu alikuwa akisikiliza maneno yale kwa umakini huku akionesha masikitiko makubwa licha ya umri wake kuwa mdogo mambo yaliyoikuta familia yetu yalimfanya kuelewa vitu vingi juu ya ulimwengu huu usokuwa na hatia zaidi ya kuwabeba watu wasio na utu kabisa.
Nilikumbuka kuwa nilikuja na vijizawadi kadhaa niliamua nimtolee mdogo wangu na mama kwani nilijua waliamini mimi ndiye furaha iliyobaki kwao na mategemeo makubwa yalikuwa kwangu.Mama alinishukuru sana nilipompa kitabu cha hadithi kwani alikuwa mpenzi sana wa kusoma simulizi mbalimbali.Mara nyingi baada ya chakula cha mchana alikuwa akimsomea mdogo wangu simulizi mbalimbali za magazetini na vitabuni yote ni kuleta furaha iliyopotea kwani walionekana kukosa marafiki wengi kama awali na waliokuja pale ni kwa ajili tuu ya kuwachunguza ili kupeleka maneno kwenye vilinge vya majungu na utetaji.Japokuwa nilimpa simu nzuri yenye uwezo wa kuonesha video za mitandaoni na kupiga mziki ambayo nilinunua baada ya kubana fedha ya bodi tupewazo chuoni alionekana kukifurahia sana kitabu kile .
‘’Cha Shigongo tena ama Hussein Tuwa?’’aliuliza akicheka
‘’Hicho hata mwandishi simjui’’nilijibu nikicheka
‘’Sasa hata mwandishi humjui , umekiokota umenunua?’’ aliuliza mama akikigeuza geuza kitabu kile
‘’We unataka mwandishi au hadithi?’’ niliuliza nikichekacheka 
‘’Majibu yako ya mkato kama babako’’ aliongea mama, 
‘’Halafu kaka anafanana na baba’’aliongea mdogo wangu na kwenda kukaa kwenye kochi alilopenda kukaa baba enzi za uhai wake, na kuanza kumwigiza akitufanya wote kucheka.Kiukweli licha ya kuwa wachache tuliotengwa na jamii ile ilikuwa tukikutana lazima furaha ipatikane.
‘’Sasa kaka utatusomea au unataka uende uwanjani kama kawaida yako?’’ aliongea mdogo wangu
‘’Hapana sitoenda uwanjani na sasa sitocheza tena mpira ‘’nilimjibu nikionesha kusikitika
‘’Kwa nini tena mwanangu?’’ aliongea mama akionekana kushtuka kwani nilikuwa miongoni mwa magolikipa waliotegemewa sana pale kijijini.
‘Ngoja na wengine wacheze sahizi sie maveterani wacha tustaafu’’ niliongea nikilazimisha tabasamu usoni pangu
‘’ Wanadamu wasikukatishe mwanangu ,,,,,,,’’ kabla hajamaliza kuna mtu alibisha hodi, alikuwa Yusuph rafiki yangu ambaye kila asikiapo nimefika kutoka shuleni lazima aje ,aliona ni zaidi ya rafiki licha ya watu wengi kuitenga familia yetu aliendeleza mahusiano yake mazuri kwetu ilifika kipindi hadi alikosana na wazazi wake kwa sababu yetu.
Baada ya salamu na maswali ya hapa na pale mama alimweleza Yusuph juu ya uamuzi wangu wa kuacha kucheza mpira , naye alishangazwa sana na taarifa ile kwani alikuja na taarifa ya kunijumuisha kwenye usajili wa timu yetu ya mtaa kwa ajili ya ligi ya ng’ombe ambayo iliandaliwa na diwani wa kata ile.
Nilimwomba alitoe tuu jina langu na nafasi hiyo wapewe vijana wengine wenye uwezo wa kudaka pale mtaani huku nikipendekeza baadhi ya vijana ambao niliona wanafuata nyayo zangu.Sikuwaambia sababu kuu iliyonifanya niaachane na soka zaidi ya kumtaka mama atusomee kitabu kile nilichompa kwani hata nami sikukisoma ,nilisema hivyo huku nikijua miongoni mwa sababu zilizoufanya urafiki wetu na Yusuph ulitokana na wote kupenda sana hadithi.
Mdogo wangu ambaye alikuwa anafanya vitu vingine alisogea karibu na mama huku akisubiri mama aanze kusoma hadithi ile.
‘’Mimi macho yananisumbua soma basi Yusuph’’alisema mama huku akimpa kitabu Yusuph, jambo ambalo lilimfanya mdogo wangu ahamie kwa Yusuph na kumwegamia hali iliyofanya wote kucheka kwani alionekana kutaka kukaa na msomaji kwani mwanzoni tulidhani alitaka tuu kudeka kwa mamake hasa kama kuna sehemu za hadithi zitatisha kumbe sivyo hivyo.Yusuph alianza kwa kukohoa na kusoma kitabu kile akiruka kusoma utangulizi wake jambo ambalo ndilo nililolitaka.Hadithi ilichukua zaidi ya masaa mawili ambapo ilikuwa imewateka wasilikizaji wake, hasa na sauti ya msomaji ambayo ilikuwa ikichukua uhalisia wa matukio kuwafanya wasikilizaji kujiona wanashuhudia visa vilivyokuwemo hadithini. Mama alishtuka baada ya kuangalia nje ambako aliona jua limeenda sana na kagiza kameanza kuingia
‘’Me subiri kwanza nikapike ‘’aliongea huku akisimama kuelekea jikoni
‘’Mama mi sitaki chakula’’, alisema mdogo wangu huku akimweleza kwa ishara Yusuph aendelee kusoma hadithi
‘’Kama we hutaki wenzako wasile kwa ajili yako?, ngoja nikawapikie kaka zako’’ alisema huku akiwasha taa za pale sebuleni
‘’Kaka Moringe si alisema hali jioni’’ aliongea mdogo wangu ambaye hakutaka hadithi ikatwe muda ule akiamini usiku atakuwa amelala hivyo kuikosa sehemu ya hadithi ile
‘’ We umemwona Moringe tuu , kakako Yusuph unadhani anatumia mafuta kusoma lazima aongeze nguvu’’ aliongeza mama akitufanya wote tucheke
‘’Mama mimi viazi nilivyokula vimenitosha kabisa labda upike kwa ajili yako’’ alisema Yusuph hali iliyomfanya mdogo wangu afurahi na kuachia tabasamu 
‘’ Jamani wote mnakataa kula kisa hiyo hadithi yenu?, ngoja nijichemshie chai hapa kuna viazi vingi tuu vimebaki najua watu fulani fulani wanakataa kula baadaye watadai viazi.’’ Aliongea mama akinisema mimi kwani nilivipenda sana viazi vitamu ,kama mtu akiambiwa aniue kwa sumu aweke tuu humo lazima nitanaswa
‘’Ngoja niende  mama nikachemshe hiyo chai nyie endeleeni tu na hadithi yenu’’ niliongea nikiinuka kuelekea jikoni
‘’Ukija maswali yako mmeishia wapi hatutaki’’alinitania Yusuph na kushika vyema kitabu na kukisoma.Nilitoka na kwenda jikoni nilipokuwa nachukua kuni niliteleza na kutoa kilio ambacho kilisikika ndani na kuwafanya wote watoke nje na kuuliza kilichonipata.Walinikuta nipo chini huku nikilalamika kwa maumivu ya mguu.Mama alipandisha suruali yangu na alichokiona mguuni kilimfanya atoe machozi hali iliyomfanya hata mdogo wangu kulia licha ya kuwa hakuona chochote ila kilio cha mamangu kilimfanya naye alie..
Chuma kilichoshikilia mguu wangu ambao kiukweli haukuwa na thamani kama awali ambayo wengi waliamini ndiyo mtaji wangu kwa kucheza soka.
''Mwanangu nini hiki?''Aliuliza mama huku machozi yakizidi kumtoka sauti yake ilizidi kunipa uchungu nikijuta kumficha.Sikutaka kumuumiza mama yangu kwa taarifa yangu na mazoea yangu ya kwenda bafuni nikiwa nimevaa suruali na taulo begani nilijua ingeficha siri yangu.
''Nilipata ajali mama''Niliongea kwa sauti ya kinyonge ambayo nayo ilikuwa na chechembe za uchungu,wakati huo Yusuph alikuwa akiniangalia kwa uchungu mkubwa alijua kabisa isingekuwa vyema kuongeza machungu kwa mama na mwana waliokuwa pale chini.
''Ajali gani mwanangu?''Mama alizidi kuongea kwa sauti ya uchungu huku mdogo wangu akiwa anatuangalia huku machozi yakimtoka.
''Tulipata ajali safarini chuoni''Nilimjibu huku nikijaribu kuinuka nikisaidiwa na Yusuph ambaye alikuja kuniinua na kuelekea ndani.Nilisikia maumivu fulani ya mfupa lakini niliamua kujikaza kwani nilijua kulalamika zaidi kungemuumiza zaidi mama jambo ambalo sikutaka kuliruhusu litokee.
''Msihuzunike sahizi nimepona na nimeshazoea''Niliongea na kulazimisha tabasamu ambalo sikujua kama lilionekana kama ni la ukweli mbele ya waliokuwa wakinitazama.
''Kumbe hujapenda mwenyewe kuacha mpira bali shida tuu zimekulazimisha?''Aliongea mama kwa uchungu mkubwa kwani mara nyingi nilimwambia lazima mpira uje kubadilisha maisha yetu sasa mguu haukuniruhusu tena kutimiza ndoto zangu nilizokuwa naziota tangu nikiwa mdogo.Nilikumbuka kipindi kile nachaguliwa kuwa golikipa bora wa kila mashindano huku uhodari wangu wa kudaka penati ukizidi kunifanya niwe naaminiwa na kila mtu kwenye timu mara itokeapo penati,hali iliyowafanya hata wachezaji kuwa tayari kucheza rafu kwenye eneo hatari maksudi wakimwamini mtu ambaye alienda kupigiwa penati hiyo.
Katika maisha yangu ya soka niliwahi kufungwa penati mbili tuu tena siku ya fainali ya mashindano fulani lakini siku ile nilidaka tatu hicho ndicho kilichomfanya kila mtu aamini kitu kitakachonipa pesa na umaarufu ni soka na si kingine na hata shuleni nilikokuwa naenda nilienda nikiamini kupitia huko ningeweza kupata timu lakini hata kabla ya kujiunga na timu ya daraja la kwanza ambayo ilikuwa Mjini Moshi nilikuwa nimepatwa na kitu kilichozima ndoto zangu.Licha ya timu ile kunitaka niitumikie huku nikiwa chuoni nilikataa na kuwataka wanitumie kipindi cha likizo ama nikimaliza jambo ambalo walikubaliana nalo huku nikishiriki kwenye michezo ya kirafiki iliyofanyika mwisho wa wiki.
Ajali ilizima ndoto zangu jambo ambalo lilinifanya nitafute kitu kingine cha kufanya ili kuboresha maisha yetu na kuwapa mama na mdogo wangu furaha ya kweli.Niliamua kuandika vitabu vya hadithi kwa msaada wa marafiki zangu wakubwa Tumsifu Joo-Chan Kaoza, Nyemo Chilongani,Yustina Emilian,Hilda Kigola,Tamasha Paulo  na wengineo wengi ambao waliamua kunisaidia kutimiza lengo langu.Kitabu cha kwanza ndicho kilichikisomwa wakati ule nikiamini itakuwa ni sehemu ya furaha ya familia ile iliyobakiwa na upweke wa ajabu usioelezeka.
''Tuendelee na simulizi mama haya mengi yapo yataisha tuu siku moja'Niliongea nikimtaka Yusuph asome kitabu kile lakini alionekana kuwa mwenyeengi pelekea kumnyang'anya kitabu kile na kukisoma kwa sauti ila na hisia za hali ya juu .

''SHUKRANI ZANGU PIA KWA MAMA YANGU MZAZI Kalista Haule na mdogo wangu mpenzi kwa kuwa sehemu ya furaha maishani mwangu.

''MUNGU HUWEKA NJIA NAJUA NDOTO ZANGU ZA KUSAIDIA FAMILIA YANGU ZITATIMIA’’.
Asanteni sana .
Moringe Jonas Mhagama.

Ilisomeka sehemu ya mwisho ya utangulizii wa hadithi ile ambayo iliwafanya waliokuwa wakinisikiliza wacheke na kuninyag'anya kitabu kuona kama yaliikuwa ya kweli.
''Kweli!'' aliongea mama kwa mshtuko mkubwa na kuja kunikumbatia akitoa machozi ,machozi ambayo kwa wakati huu yalikuwa ya furaha si kama awali alipoona chuma mguu mwangu.
''Mwanangu mshukuru Mungu kwa vipaji alivyokupa ulishindwa amekuleta huku''Aliongea mamsauti ambay kama ya kilio ama kicheko.
''Umezoea kuona machozi yangu mwanangu,lakini chozi hili ni tofauti na machozi mengine hili ni CHOZI LA FURAHA MWANANGU''Aliongea kucheka kwa sauti iliyowafanya hata Yusuph na mdogo wangu wacheke na kunipongeza.
     MWISHO............



Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends