Taswira; Tafrija ya mchapalo baada ya Tigo na samaki samaki kuingia Ubia yafana

on Tuesday, May 3, 2016 - No comments:

Wadau wakifurahi usiku wa jana wakati wa hafla ya mchapalo baada ya Tigo na mgahawa wa samaki samaki kuingia Ubia ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja  kwa kuleta  bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.

Vinywaji murua kabisa 

Warembo wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja na wageni waalikwa wote 

Ulinzi ukiimarihwa kwa  wageni waalikwa na  wateja wote

Mtaalamu wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar (kulia ) akiwa katika pozi na wafanyakazi wenzake Ummy Mtiro na Natasha 

Mhudumu wa Samaki akitabasamu na kuwakaribisha wageni waalikwa 

Blogger na mdau wa mitandao ya kijamii John Kiandika akiwa katika pozi na mkewe wakati wa hafla usiku wa jana 

Mmoja ya wageni waalikwa akipata maelezo kuhusu huduma ya Tigo 4g kutoka kwa mhudumu

Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos

Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout akifurahi jambo na wafanyazi wa tigo wakati wa hafla hii

Watangazaji maaruf wa kituo cha Clouds tv Hudson Kamoga na Sam sasali wakiwa pamoja kupata maelekezo kuhusa huduma ya intanet ya kasi ya Tigo 4G kwenye hafla hiyo.


Mhudumu akiandaa chakula 

Wahudumu wa samaki samaki wakiwa katika pozi 

wadau wakiwa katika pozi 


Taswira ukumbini 

Mdau John kiandika na mkewe wakipata maelezo zaidi kuhusu huduma ya Tigo 4g 


wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja 



Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania,

ikijulikana kama“nembo ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”.

Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedhaza kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music ( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.

Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na Hivi karibuni Tigo imezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar es Salaam nzima, na unatarajiwa kuzindualiwa nchi nzima.  Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya minara mapya 500 yenye mtandao wa Tigo nakufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongezauwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini.  

Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 10 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwawateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.

 Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni ya Millicom, kampuni ya kimataifa  inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 11 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na Amerika yaKusini na ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani.








Kuhusu Samaki Samaki
Ukiwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula  vinavyotokana na mazao ya baharini  na vinywaji  nchini Tanzania, Samaki Samaki  inamiliki migahawa mitatu  ambayo ipo Mlimani City
(Ubungo/Mwenge), City Centre (kwenye makutano ya Barabara ya Samora na Mirambo) na Samaki Samaki  kwenye Barabara ya Haile Selassie.
Tangu kuanzishwa kwa tawi la Mlimani City mwaka 2007 tumeshuhudia kupanuka kwa  Migahawa  ya Samaki Samaki  hadi matawi miwili  zaidi ndani ya jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wake,  kuongezeka kwa wateja ambao wanafikia hadi 1,000 kwa siku ndani ya matawi hayo,  kuongezeka  kuimarika  kwa nembo yetu ya biashara  na kutambuliwa na umma,  kupatikana kwa fursa za ajira kwa wazawa, jamii kutuunga mkono kupitia Mfuko wa Samaki Samaki ( Samaki Samaki Foundation) ambao unalenga kuwasaidia  wahitaji  kwa kutoa misaada ya kuwajibika kwa jamii,  jamii imeweza kutufikia  kwa kutumia  video na muziki uliorekodiwa  katika kukuza  nembo yetu kupitia Samaki Samaki Fleva na kuuza  bidhaa zetu nyingine  ambazo hazihusiani na chakula  zikiwemo kofia, fulana  na CD za muziki.

 Dira ya Samaki Samaki ni   kushikilia nafasi yake  nchini Tanzania  kwa kukua hadi mikoa mingine nchini  na hata baadaye  kusambaa hadi  kona nyingine za Afrika na dunia kwa ujumla. Kwa hivi sasa  inaangalia Mwanza na Arusha  kama vituo vya kuanzia kusambaa hadi mikoa mingine.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends