Diamond Platnumz aelezea jinsi alivyoweza kupata kolabo wakati anatoka kimuziki

on Friday, August 5, 2016 - No comments:

Msanii Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa kabla ya yeye kutoka kimuziki kuna wasanii watatu wakubwa aliwalipa pesa ili afanye nao kazi katika kutafuta yeye kutoka kimuziki.


Diamond ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema alishawahi kumlipa Mr Blue elfu sitini, marehemu Albert Mangwea alimlipa shilingi elfu hamsini pamoja na Fatma mdogo wake na msanii Hard Mad .

"Kabla sijatoka niliwahi kuwalipa wasanii wakubwa kipindi hicho ili nifanye nao kazi, niliwahi kumlipa Mr Blue, Arbet Mangwea pamoja na Fatma, lakini kati ya wote hao msanii Chid Benz Chuma huyu jamaa yeye kwanza hakuwahi kunisumbua kwenye collabo, lakini pia hakunilipisha hata kumi, yaani sikuamini kabisa vile nilivyokuwa namsikia na nilipompigia simu na alivyonipokea ilikuwa tofauti sana" alisema Diamond Platnumz

Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends