|
Hili ni eneo la Ruvu darajani likiwa limefurika maji hadi kwenye kingo za mto |
Kutokana na mvua kali zinazoendelea kunyesa mkoani DSM na mikuoani kumekuwa na madhara makubwa sana hassa kwa upande wa miundombinu ya barabara. Mvua hizo zimesababisha kufungwa kwa barabara nyingi sana hapa mjini kutokana na maji kujaa na kukatisha juu ya madaraja. Siku ya jana haikuwa nzuri kwa upande wa Bagamoyo kutokana na kuvunjika kwa kuta za daraja linalounganisha mji huo na jiji la DSM, lakini leo imekuwa ni siku mbaya zaidi kwani jiji la DSM litakosa mawasiliano na mikoa yote na nchi za jirani zinazotegemea usafiri huo kutokana na kuzuiwa kwa magari kuvuka daraja hilo ili kuepusha maafa ambayao yanaweza kutokea.Kwa taarifa tuliyonayo hakuna gari linaloruhusiwa kupita na kuna msongamano mkubwa sana wa magari na wato katika eneo hilo inawapa Pole sana watanzania kwa hali mbaya na adha mnazozipata kutokana na mafuriko haya.
0 comments: