Lazaro Nyarandu
Zito Zubery Kabwe akiweka taji la maua katika kaburi la Rafiki yake mpendwa Deo Filikunjombe, leo jioni
SPIKA wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda amesema kuwa Mbunge marehemu Deo Filikunjombe, alikuwa ni mbunge wa tofauti kutokana na alivyo kuwa akifanya kazi zake na alikuwa hakai bungeni alikuwa anapenda kukaa na wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Spika Makinda alisema kuwa Filikunjombe alikuwa ni mbunge wa tofauti na alipenda kuwa na wananchi mda wote na kila alipokuwa akimaliza bunge alikuwa anakimbilia kwa wananchi wake.
Alisema kuwa alikuwa ni mpiganaji kwa kufanya kile anacho kiamini serikali inaenda tofauti hukipigia kelele na huhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Alisema kuwa wananchi wamempoteza mpigania haki zao na wahakikishe kuwa wanaangalia mbunge atakeye kuwa tayari kumalizia mipango yao aliyo kuwa ameianza mbunge wao.
"Filikunjombe alikuwa ni mbunge jasiri na alikuwa akiwatetea WanlLudewa na Watanzania kwa ujumla.
Aliongeza kwa kutoa wito wa watu wanao litaka jimbo la Ludewa kuhakikisha kuwa wanakuja kutekeleza yale aliyo kuwa ameyaanza Deo na kukamilisha mipango yake huku akisema kuwa mbunge huyo alikuwa na mipango ya miaka mingi kuifanya Ludewa ya tofauti.
Alisema kuwa Deo alikuwa ni mbunge mwenye kupenda maendeleo na kuleta umeme katika jimbo hilo pamoja na barabara za kufika katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Aidha wa upande wake Rafiki yake mpendwa Wa Filikunjombe, Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zito Kabwe amesema kuwa anasikitika kutokea kwa msiba wa rafiki yake mpendwa na kuwa hatoweza kumpata rafiki wa aina ya Filikunjombe kutokana na alivyokuwa.
Alisema kuwa kwa wakazi wa Ludewa wamempoteza mtu muhimu sana na kuwa hawata kuja kumpata mbunge kama huyo licha ya kuwa watapata mbunge lakini kufanana na Deo ni vigumu.
Aliongeza kuwa Deo kwakuwa aliwapenda Wanaludewa wakati ajali inatokea alijaribu kuruka na mwili wake ulikutwa mbali kidogo na mabaki ya ndeke inaonekana alikuwa anataka kujiokoa na kuungua na moto uliokuwa ukiwaka kutoka ilipo angukia Ndege.
Akihubiri katika ibada ya mwisho ya msiba wa marehemu hao watatu ambao ibada ilikuwa ni moja Askofi wa Kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombe, Ask. Alfred Maluma alisema kuwa msiba huo ni mkubwa kwa kuwa umehusisha watu watatu wanao tokea sehemu moja na kuwatia moyo wafiwa kwa kuwaambia kuwa wawe wavumilivu katika siku hizi ngumu kutokana na msiba wenyewe ulivyotokea na ughafla wake.
Akielezea safari ya kuja kutoka Mjini Njombe kuelekea wilayani Ludewa alisema kuwa walikuwa wakisimamishwa kila mahali na wananchi wakilia kuonyesha masikitiko yao juu ya kifi ya Filikunjombe.
Alisema kifo chake kimewashitua wengi kutokana na alivyo kuwa akiwasaidia wananchi na kuwa wananchi katika vijiji mbalimbali walikuwa wakilia kwa sauti licha ya kupita Usiku katika maeneo hayo.
Mwili wa marehemu uliwasili usiku majira ya saa 7 usiku katika mji wa Njombe baada ya kufanya ibada katika kanisa katiliki Njombe mjini na kuanza safari kuingia nyumbani kwao Mjini Ludewa. Ibada ya kuwaaga Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake Egid Nkwera, Casablanka Haule ambao walikuwa wakisafiri kwa pamoja kutoka jijini Dar Es salaam kuja mkoani Njombe ilifanyika leo siku ya jumapili na kumalizikia katika makaburi ya Ludewa Mjini.
Msiba huo ambao umekuwa mkubwa kwa wakazi wa Jimbo la Ludewa ulio kusanya umati mkubwa wa wakazi wa Ludewa na watu kutoka sehemu mbalimbali maduka katika mji wa Ludewa yalifungwa kwa siku mzima huku wakazi wa mji huo wakiomboleza msiba wa mbunge wao.
Katika msiba huo kuna viongozi mbalimbali waliofika kuomboleza akiwemo Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu, Wiliamu Lukuvi, na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi wa nyadhifa mbalimbali.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Wilayani Ludewa wamesema kuwa hawatampata mmbunge mweye aina ya mbunge wao na kuwa Msiba huo umetokea kwa ghafla wamesikitika sana ni bora angeumwa wangejua anaumwa.
Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga na mgombea wa ubunge jimbo la Makambako alisema kuwa Jumapili iliyopita alikuwa katika jimbo hilo kupiga kampeni kumsaidia marehemu anasikitika kutokea kwa msiba huo, huku akibubujikwa na machozi alisema kuwa alipiga kampeni katika vituo saba na kuwa aliagwa na mgombea huyo jumanne iliyopita alimuaga kuwa anaenda Dar es Salaam.
WASTAREHE KWA AMANI NDUGU ZETU WAPENDWA, MBELE YETU NYUMA YAO,
AMEN.
0 comments: