Jimbo la Ludewa ni moja kati ya majimbo ambayo wananchi wake hawakuweza kupiga kura kumchagua mbunge wao katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2015 kutokana na mmoja wa wagombea kupitia Chama cha Mapunduzi kufariki dunia baada ya kupata ajari ya chopa.
Kwa muda kidogo Wanaludewa wamekuwa wakitafakari ni nani kuwa mrithi wa kipenzi chao Deo na siku za hivi karirubuni wameweza kujitokeza watia nia kadhaa kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi akiwemo mdogo wa marehemu Deo, Filipo Filikunjombe, Eng. Chaula, Mstaafu Mpangala, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji), Deo Ngalawa na wengine.
Siku ya jana ndiyo ilikuwa siku ya kufunga kazi ndani ya chama cha Mapinduzi ili kumpata mtu mmoja atakayekiwakilisha chama hicho. Baada ya masaa kadhaa ya upigaji kura na uhesabuji wa kura uliofanywa na wagombea wenyewe (kama tulivyopata taarifa kutoka chanzo kimoja mtandaoni) ndipo matokeo yakawa kama ifuatavyo:
- Deo Ngalawa 537
- Philipo Philikunjombe 501
- Mpangala 03
- Emmanuel Masanja 19
- James Mgaya 72
- Evaristo Mtitu 21
- Chaula 38
- Na zilizoharibika ni 2
Kwahiyo kwa matokeo hayo yanamuwezesha bwana Deo Ngalawa kuwa mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM.
Mwisho wa safari moja ndio mwanzo wa safari nyingine, ya kuelekea Bungeni.
0 comments: