Mkazi mmoja wa kijiji cha Ludewa Mjini anayejulikana kwa majina ya Nickolaus Haule katika kata ya Ludewa wilayani Ludewa mkoani Njombe siku ya jana amepelekwa mahabusu kwa tuhuma inayomkabili ya kum' baka mbuzi jike katika eneo la Ipogo.
Akisoma shitaka hilo mbele ya ASP Emmanuely Mtairuka mbele ya hakimu Jokim Mwakyolo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kumbaka mbuzi huyo mnamo januari 01 mwaka huu majira ya saa nane na dk 45 mchana siku ya mwakampya 2016.
Aidha shtaka hilo linamkabili mkazi huyo kutokana na kukiuka kifungu cha sheria namba 154(1)b na kesi yake itasikilizwa tena january 11 mwaka huu.
0 comments: