What's New Here?

Showing posts with label Daniel Burton Mwaseba. Show all posts

Kwa utafiti mfupi na wa haraka nimegundua nchi ambazo ‪raia‬ wake ni wachapakazi ndizo zenye maendeleo makubwa duniani. Hivyo nikakumbuka ile tafiti ya watu, sikumbuki taasisi gani waliyofanya wakasema katika Afrika mashariki ‪‎Watanzania ndio huongoza kwa matumizi ya mitandao ya kijamii. Ndipo nikafanya connection kati ya maendeleo na mitandao ya kijamii na kuwaza labda Tanzania hatuna maendeleo makubwa kwa sababu ya matumizi makubwa na hasi ya mitandao ya kijamii inayopelekea kusifanyike kazi za kimaendeleo ipasavyo.

Nikawa natafuta mfano mahususi na kupata mfano ambao unathibitisha hilo. Mfano niliyoichukua ni katika kundi moja la WhatsApp nililoachana nalo baada ya kukaa kwa muda wa wiki mbili tu. Kwanza niliona ajabu sana siku za kazi (Jumatatu - Ijumaa) watu wako bize kuchati mambo yasiyokuwa na maana na wanachangamka kweli kweli. Lakini siku za wikendi walikuwa kimya kabisa, ndipo nikajithibitishia kuwa laiti kama ule muda mrefu wa kuchati ungekuwa unatumika ipasavyo kwenye kazi ninauhakika uzalishaji mali na huduma ungekuwa mkubwa sana katika sekta zote yaani binafsi na serikalini. Pia kungekuwa na ufanisi mkubwa sana katika kazi kwani muda wa kazi watu wangefanya kazi kwa umakini zaidi na muda wa mapumziko baada ya kazi na siku za wikendi zingetumika kuchati.

NB: Time management is a vital factor for sustainable Development

Matumizi ya mitandao ya kijamii na maendeleo ya Watanzania/Tanzania

Kuna uwezekano umeshaandaa vyeti vyako na wasifu wako na upo kwenye michakato ya kuanza kuzunguka na bahasha kupeleka sehemu mbalimbali ii kuomba nafasi ya ajira. Kabla hujaweka nguvu na matumaini yako kwenye mchakato wa kuzunguka na bahasha kuna vitu vichache ambavyo ni vyema ukavijua.

1. Nafasi za ajira ni chache kuliko idadi ya wahitimu na wenye sifa. Kwa sasa karibu kila kada ukiondoa elimu na afya kuna nafasi chache sana serikalini na hata kwenye taasisi binafsi. Hata kwa kada ya elimu nako kwa miaka ya hivi karibuni kuna baadhi ya wahitimu wamekosa nafasi za kazi. Hivyo unavyoingia sokoni jua kabisa ‘demand’ ni ndogo kuliko ‘supply’

2. Sio kila nafasi za kazi zinazotangazwa ziko wazi. Kuna baadhi ya taasisi zinatangaza nafasi za kazi ili tu kutimiza wajibu na sheria ya kutaka ajira zitangazwe kwa umma. Hivyo unaweza kuandika maombi, ukaitwa kwenye usaili na bado ukaambiwa umekosa nafasi.

3. Wenzako wa mwaka jana na mwaka juzi bado wanazunguka na bahasha. Bado kuna wahitimu wengi wa miaka iliyopita nao bado hawajapata ajira. Kuna ambao bado wanaendelea kupitisha bahasha na kuna baadhi ambao wameamua kufanya mambo mengine. ni vyema kuwatafuta wa kila kundi ili ujifunze machache kutoka kwao.

4. Mishahara ya kazi za kwenye taasisi binafsi ni midogo sana. Tofauti na story za vyuoni kwamba mishahara inaanzia labda laki tano au laki saba jua kuna wenzako wana degree hivyo hivyo na wanalipwa laki mbili. Kama ukipata kazi na mshahara wakakutajia mdogo kama huna kingine cha kufanya ni bora kuchukua kazi hiyo ila uifanye kwa lengo la kupata ujuzi na kujenga mtandao na watu wanaofanya kada uliyosomea. Kuliko kukaa mwaka mzima ukizunguka na bahasha ukitegemea mshahara mkubwa ni bora kupata japo laki mbili kwa mwezi huku ukiendelea kukuza mtandao wako na ujuzi wako.

5. Kuna kazi za kujitolea, kama umekosa hata kazi ya bei rahisi kuna taasisi nyingi ambazo zina mpango wa watu kujitolea kufanya kazi na baadae unaweza kuingizwa kwenye ajira. Kama hali ya nyumbani inaruhusu kwa kuweza kupata kula na nauli fanya kazi za kujitolea na huko onesha uwezo wako na vipaji vyako. Kwa kuonesha uwezo na vipaji ni rahisi sana kukubalika na kupewa nafasi, na pia utatengeneza mtandao wa watu watakaokuonesha njia zaidi.

6. Sio lazima ufanye kazi ya kitu ulichosomea. Kuna baadhi ya kazi zinaweza kufanywa na mtu yeyote aliehitimu elimu fulani. Kwa mfano kwa sasa kuna uhaba mkubwa wa walimu, hivyo kama umehitimu unaweza kutafuta shule na ukafundisha masomo yanayohusiana na ulichosomea. Kama umesoma kada za biashara unaweza kufundisha masomo ya biashara, kama umesoma sayansi kuna nafasi kubwa za kufundisha masomo ya sayansi kutokana na uhaba wa waalimu wa sayansi. Kama unadhani kushika chaki sio hadhi yako basi endelea kuzunguka na bahasha mjini.

7. Angalia mazingira yanayokuzunguka na jinsi unavyoweza kuyatumia kutengeneza ajira kwako na kwa wanaokuzunguka. Hii ndio dhana halisi ya elimu ila kwa kuwa elimu yetu inatuandaa kuwa waajiriwa basi tunajikuta wote tunasubiri kuajiriwa.Ni vyema ukaanza kufikiri tofauti na uliyofundishwa chuoni kuhusu ajira.

8. Cha mwisho kabisa ambacho ni vyema ukakijua na ambacho ingebidi kiwe cha kwanza ni kufanya maamuzi ya kujiajiri. Kama utachoshwa na kuzungusha bahasha ama kama hutaki kupata hiyo karaha ni vyema ukafanya maamuzi ya kutotegemea kuajiriwa. Tumia uwezo na vipaji ulivyonavyo changanya na elimu uliyoipata halafu tumia mazingira uliyopo kutengeneza ajira kwako na kwa wanaokuzunguka.

KABLA HAUJAANZA KUZUNGUKA NA NA BAHASHA YENYE CV NA VYETI ILI KUFUKUZIA AJIRA PATA ELIMU YA BURE

Like, share and send to friends

Jiunge nasi