Kwa mara nyingine nchi ya Tanzania imeingia katika historia ya dunia. Moja ya maeneo ambayo yataona kupatwa kwa jua kwa asilimia zaidi ya tisini ni kutoka Tanzania eneo la mkoa wa Njombe na Mbeya, Nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Katika kijiji cha Litundu kilichopo katika wilaya mpya ya Wanging'ombe tayari uongozi kutoka ngazi mbalimbali za serikali umefanya maandalizi ya kuwapokea wageni watakaoelekea maeneo hayo ili kujionea tukio hilo ambalo hutokea kwa nadra sana katika sayari ya dunia na inasemekana litatokea tena ifikapo mwaka 2096 au 2097. Tukio la kupatwa kwa jua katika eneo hilo litatokea saa tatu na dakika tatu na sekunde 56 (03:03 asubuhi) na litadumu kwa muda wa dakila tatu na sekunde tano nukta sita (03m5.6s). Pia wametoa angalizo kwa wananchi wa maeneo hayo juu ya athari wanazoweza kuzipata kwa kuangalia jua bila kutumia vifaa maalumu.
Pia kutoka mkoa wa Mbeya eneo la Mbarali ndio eneo pekee ambalo watashuhudia tukio hilo kwa uzuri kabisa.
0 comments: