Tigo yazindua huduma ya kipekee ya Tigo Games

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiongea na waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa  huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games jijini Dar Es Salaam jana.Tigo Games ni huduma katika wavuti  ambayo imesheheni  michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenye simu za Smartphone au Tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakua App ya Tigo Games.


Wasanii wakiigiza kama Mazombie katika kunogesha uzinduzi wa TIGO GAMES


Wasanii wakicheza mpira katika uzinduziwa tigo games mapema jana katika ukumbi wa High Spirit Jijini Dar es salaam


Wadau mbalimbaliwakipata taswira mbele ya gari katika RED carpert 
Wasanii wakiwa katika pozi na mfano wa Risasi katika uzinduzi wa TIGO GAMES 


Wadau wakifurahi jambo katika uzinduzi huo


Mtangazaji wa Choice Fm na Mchekeshaji Idris Sultan akiwa live jukwaani kusherehesha uzinduzi wa Tigo Games mapema jana katika ukumbi wa High spirit Jijini Dar es Salaam


Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akifurahi jambo na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) wakati wa uzinduzi 
Wasanii wakitumbuiza nyimbo za michael JacksonMfanyakazi wa Huawei akielekeza jinsi ya kucheza Games hizo mbalimbali zinazopatikana katika Tigo Games 


Baadhi ya wadau wakipata maelekezo jinsi ya kuingia katika mashindano ya kucheza Games na mshindi kujishindia Zawadi


Waadndishi wa habari wakishindana kucheza Games katika uzinduzi wa Tigo Games jana usiku 


Msanii wa kizazi kipya Benpol akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa clouds tv Perfect baada ya uzinduzi wa tigo games


Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Tigo Games mapema jana usiku
Wadau wakipata picha katika sanamu za michezo ya Tigo Games 


Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Tigo Games 
Dar es Salaam, Mei 192016- Kampuni ya simu inayoendesha maisha ya kidijitali Tanzania, Tigo, leo imetangaza uzinduzi wa huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games. Tigo Games ni huduma katika wavuti  ambayo imesheheni  michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenyeSmartphone au tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakuaApp ya Tigo Games. Kwa wateja wenye simu za kawaida zilizo na intaneti watapata huduma hii katika tovuti ya Tigo Games.
 Michezo zaidi ya 800 inapatikana kupitia huduma hii ikiwemo michezo maarufu ambayo ni pamoja na Buddy Man, Cut the Robe, Zombie Run na Tokyo Drift.
 Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa huduma hii mpya jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Huduma hii mpya ya  michezo  inaifanya Tigo kuwa ya kwanza katikamitandao ya simu Tanzania  kutoa jukwaa la michezo linaloweza kutumiwa  na watu wengi ambapo wateja wa Tigo  wanaweza kucheza michezo mbalimbali  kulingana na chaguo lao kwa gharama wanayoimudu. Tigo imejikita kuendelea kusimamia maslahi ya wateja wake kwa kutoa  bidhaa nyingine nyingi  kwa ajili ya manufaa ya kuwa na simu za kisasa.”
 “Tigo sasa ndio inaongoza katika upatikanaji wa huduma ya 4G LTE nchini, na kwa sasa huduma hii inapatikana katika miji mikubwa 12. Tunaamini kwamba wateja wetu watafaidika sana kutokana na intaneti yenye kasi zaidi itakayo wawezesha kupakua na kucheza michezo hii,” alisema Gutierrez.
Tigo Games ni huduma ambayo mteja akichajua kulipia mara moja, ataweza kuchagua michezoaipendayo na kuicheza atakavyo wakati wowote.  Kuna VIP Club ambayo inampa mteja uamuzi wa kujiunga na kifurushi cha siku, wiki na hata mwezi; pia kinamruhusu mteja kupakua michezo bila kikomo.
Mteja ataweza kucheza michezo kwa mda wowote autakao bila makato yeyote. Malipo ya utumiaji wa data kadri mteja anaendelea kucheza ndio yatakayo hitajika. Uzinduzi wa VIP Games Club utakapofanyika, siku 7 za mwanzo wateja wataweza kufurahia huduma bure kwa kutembelea wovuti huu: http://burudani.tigo.co.tz/games

“Kuanzishwa kwa bidhaa hii  kupo kwenye mikakati ya Tigo  ya kuwapatia wateja wake  bidhaa na huduma zilizo na ubora duniani  ambazo  zinawawezesha  kufurahia kwa ujumla maisha ya  kidijitali,” alisema Gutierrez.

HUU NDIO WIMBO WA JUMUHIYA YA AFRIKA MASHARIKI USIKILIZE HAPA

Wiki chache zilizopita serikali ilitoa alama rasmi za jumuhiya ya Afrika ya mashariki ambazo zitatumika na kuwekwa katika ofisi za serikali na shughuli nyingine ziihusuyo jumuhiya hiyo.
Usikilize wimbo wa jumuhiya hii hapa chini share pia wenzako wausikie na kufahamu wimbo wa jumuhiya yetu tukufu;

Isack - Nitulie (Produced by Ventskillz-Kwanza records)

Mziki mtamu umerudi mahala pake. Isack ambaye mwanzo alikuwa akifanya mziki wake chini ya studio yake ya Icon records sasa kafanya mziki huu mzuri chini ya Kwanza records. Wimbo unaenda kwa jina la "NITULIE" umefanywa na mtayarishaji midundo Ventskillz kutoka Moro town. Isikilize na kuipakua ngoma hii mpya 

Usiku wa Lady Jaydee jinsi ulivyofana ndani ya Mlimani City


Lady Jaydee akiwa anawapa burudani mashabiki waliokuwapo mlimani city kwa wingi

Rama Dee akiwa Lady Jaydee

Alikiba naye akukosa, alipanda jukwaani kuwasalimia mashabiki

Mh. Esther Michael Mmari kufikisha kero za wanafunzi wa NIT bungeni

Wakimsikiliza kwa makini Mh. Esther MmariMh. Esther Michael Mmasi amefanya kikao na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Bungeni Dodoma. Jambo kubwa lilikuwa ni kupata kero na changamoto zinazowakumba wanafunzi wa Chuo hicho zinazohitaji kusemewa ndani ya Bunge na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
(Pictures fromFacebook account Esther mmasi)

Video: Mayunga ft Akon – Please don’t go away

Mshindi wa Trace Music Star kutoka, Tanzania Mayunga ameachia rasmi video mpya ya single yake mpya aliyomshirikisha staa Akon inaitwa ‘Please Don’t go away’.

Video: G Nako Ft Chin Bees & Nikki Wa II – Arosto

Msanii kutoka kampuni ya Weusi G Nako ameachia video mpya ya Single yake ya “Arosto”, G Nako ameachia video hiyo aliyowashirikisha Chin Bees na Nikki wa Pili.
Video hii imefanyika mara mbili baada ya video ya kwanza kufanya na Nisher na hii ya pili iliyoiachia imefanywa na directora Hanscana,

NI NEEMA BAADA YA NEEMA VIDEO MPYA YA ALIKIBA INA HILI USILOLIJUA

Baada ya kupata mkataba mnono wa Sony Music global na kuwa balozi wa Jamie Food revolution huku akitegemea kuwa kwenye ukurasa wa mbele kabisa wa jarida la The source Magazine.Video yake mpya ya Aje imepokelewa kwa nguvu na mashabiki wengi duniani jambo ambalo huenda likazidi kumpa mikataba mingine. Hadi sasa video hiyo ndani ya saa ishirini na nne imetazamwa na watazamaji;209,511 na wamekuwa wakiongezeka kwa kasi sana, itazame video yake hapo chini

Haya ndiyo niliyoyaona baada ya kusikiliza "Moyo mashine"


Juzi wakati nikizurura kwenye kurasa za wanamuziki nchini nikajikuta nikiangukia twitter kwenye ukurasa wa mwanamuziki Ben Poll, hapo nikaziona post zake zikiwa na hashtag ya moyo kazi yake nini. Hapo nikajikuta nitafakari sababu ya hashtag hiyo nikaisearch lakini nikakuta ni yeye ndiye aliyeileta. Akili yangu ikafanya kazi haraka.
Wimbo mpya.

Naam sikukosea kwani dakika chache baadaye nikiwa redio nikasikia akihojiwa nini maana ya hashtag hiyo, jibu lake likawa ni wimbo mpya kama nilivyodhani.Nikaanza kuhisi ulikuwa ni wimbo aliudharau kwa kuamua kuwashtukiza mashabiki na wapenzi wa muziki. Huenda ni buns track isiyo na madhara makubwa, nikahitimisha na kuendelea na harakati zangu za kusaka umbea. Ndiyo kusaka umbea kama nisipoujua umbea nitaandika nini mwanakalamu maana mie umbea wako unaokuaibisha kwangu ni naugeuza fursa na darasa wakati mwingine ni fimbo ya kuwanyoosha wasiokuwa wastaarabu.
Usiku nilikuta link ikisambaa kila mtu akiusifia wimbo wa mkali huyo wa Rnb, nikaupakua huo wimbo na kuusikiliza.neno la kwanza kunitoka lilikuwa ni kwamba huu wimbo angeimba na Baraka Da Prince neno la pili lilikuwa ni kuwa kama nasikia ile radha iliyopotea ya Kid bway naikaamua kufuatilia mtayarishaji , sikukosea alikuwa ni Lolly Pop yule yule mwimbaji wa Injiri na mtunzi wa nyimbo kali za bongofleva na mpishi ama muuandaaji wa nyimbo halisi za bongofleva.Nyimbo ambazo ukizisikia popote utajua ni za kutoka Tanzania nchi ya bara na visiwa kadhaa.

Hapo nikagundua mambo yafuatayo;
Ben Paul ni mwanamuziki si msanii,
Ukiangalia video yake unaweza kuhisi huyu jamaa hana swag kama wenzake katika bongofleva wafanyavyo maana hakuna gorofa wala vinguo vya kuweka maungo ya wanawake nje.Lakini licha ya huko kukosa kwake swaga Ben paul hajaweka usanii sana kwenye kazi yake bali uanamuziki unaonekana na hata wimbo wenyewe una nguvu ya kukaa kwenye charti miazi zaidi ya mitatu bila hata ya kuwa na video kama ilivyokuwa Sophia.Ben kauonesha uanamuziki wake katika kujua kupanda na kushuka kwa sauti zake huku melody za wimbo zikibeba nini mashairi yanataka.

Lolly Pop ni mkuu asiye na makuu
Kwa mara ya kwanza nilianza kujua utunzi wake pale niliposikiliza kwenye Basi nenda, wimbo ambao pia aliuandaa lakini sikuzikia akijitapa kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni zaidi ya Mo Music kama watunzi wengi wanavyozuka baada ya wimbo wao walioutunga ukiwa mkubwa.Nilikuwa namsikiliza wakati anhojiwa na Saida Mwilima , kwa upole bila makuu alikuwa akiutambua na kuuheshimu uwezo wa waimbaji anaowaandikia nyimbo.Hata aliandika nyimbo za Baraka Da Prince hakuonekana kuutamani umaarufu ambao Baraka angeupata baada ya ngoma hizo kuwa kubwa bali alibaki mkimya na mwenye kuchagua maneno ya kusema pale alipohojiwa huku akijivunia kuwa mwandishi wa nyimbo za wanamuziki wenye vipaji.
Ni busara ilioje.

Lolly pop ambaye jina lake la kwenye vitambulisho ni Godluck mwimbaji wa nyimbo kadhaa za injiri ukiwemo ule wa ‘’Acha waambiane’’ bado hajaonesha tama ya kuwa maarufu huenda angekuwa mwingine angeamua kuachana na kuimba nyimbo za injili na kuhamia kwenye bongofleva anabaki kuwa mkuu asiye na makuu.
Kuna kipindi niliwahi kusoma mahali kuwa alikuwa tayari kumwandikia Alikiba wimbo buree kabisa.

Kidy Bway ni mkali wa kachumbali na melody kali
Kwa sasa ni mmoja wa wafanyakazi wa kituo kipya cha redio ya jijini Mwanza Lake fm , kabla ya hapo alikuwa Sahara Media kabla ya kwenda Bongo five.Pia ni mtayarishaji wa muziki katika studio ya Tetemesha Record aliwahi pia kuwasimamia wanamuziki Sagna,Csir madini na Baraka Da Prince kwa nyakati tofauti pia ni moja kati ya watu ambao walichangia mafanikio ya kimuziki ya Hussein Machozi.

Kidy ni mkali wa kuweka kachumbali kwenye nyimbo zinazopitia mikononi mwake kama huamini tafuta nyimbo zote zilizopita tetemesha records pia licha ya ukali wa kutia kachumbali kwenye nyimbo hizo Kidy ambaye jina lake la kitambulisho ni Sandu George Mpanda anazalisha kazi zenye melody kali kitu kinachofanya wimbo kuwa na maisha marefu kwenye maiskio na akili za watu.

Moyo mashine ni wimbo wa kumwimbia ama kumdedicate kipenzi chako, kwa kipindi hiki anaweza toa chozi la furaha.
#BenPolumetunyoosha.
Niambie ulichokiona kwenye Moyo mashine ya Ben Paul, niandikie hapa chini.

Oktoba ya ule mwaka


Na.Mwanakalamu
Tanu wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba mwaka ule iikuwa ni wiki ngumu sana kwa baba, alikuwa habanduki kwenye redio hata pale nilipompigia kelele ama kumsumbua kwa namna yoyote hakuhangaika nasi bali alijitenga na kuingia chumbani.Shuleni tulikokuwa tukisoma , akifundisha baba alikuwa akijifungia ofisini  kwake muda mrefu sana na redio yake.
Sikujua chochote kilichomfanya awe katika kupenda kusikiliza redio kwa kiwango kile huku akiwa mwenye hofu sana.Kwa umri wangu na elimu yangu ya darasa la kwanza nililokuwa nikisoma sikuona umuhimu wowote wa kujua  kilichomsibu zaidi ya kuendelea na michezo ya kitoto kutwa japo usiku niliporudi nyumbani nilikuta akiwa amenyong’onyea sana ,nikawa naogopa sana lakini sijui ndo utoto wenyewe sikujihanganisha naye sana kwani upole wake pia ulikuwa ji nafasi yangu ya kutozingatuia maagizo yake.
Jioni  ya tarehe kumi na tatu nakumbuka ilikuwa ji siku ya jumatano siku ambayo nilitakiwa kufua nguo zangu kwani siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya kukaguliwa usafi shuleni  baba yangu alionekana mwenye hofu sana.Nilipata nafasi ya kuuliza juu ya hofu aliyokuwa nayo na kumfanya awe rafiki wa redio wakati akinifulia nguo za shule ambazo hadi usiku wa saa moja na robo baada ya habari ya sauti ya Tanzania Zanzibar.
Alinijibu kwa kifupi tuu;
‘’Hali yake imekuiwa mbaya sana’’
Nilipouliza ni nani huyo , hakunijibu zaidi ya kunizuia kuongea kwani kipindi cha michezo kilikuwa kimeshaanza, name nikaungana naye kusikiliza japokuwa nilikuwa sijui chochote zaidi ya kurithishwa ule ushabiki wake wa timu ya Simba.
Siku iliyofuata nilienda shuleni nikimwacha baba pale nyumbani akiwa mwenye hofu  sana.Darasani tuliendelea na vipindi  vya asubuhi hadi pale kengele ilipogongwa kwa dhalula.Walimu wote wakiongozwa na Mwalimu mkuu (baba yangu) akiwa mwenye uchungu mkubwa akitangaza kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nilimshuhudia baba yangu akilengwa na choxzi kabla ya kuondoka akijifuta machozi  kwa kitambaa akimwacha msaidizi wake akimalizia matangazo na kututawanya akituambia tukawaaambie wazazi wetu tuu ya kifo hicho ya kiongozi huyo wa Afrika.Nakumbuka karibu darasa la kwanza wote tulianza kulia kwa sauti tukiwa hatujua kilichomliza mwalimu miuu na kuwafanya walimu wengine wawe katika simazi vile.Wanafunzi wa madarasa ya juu nao walianza kulia kwa sauti ya chini lakini wanafunzi wengi wa kike walilia kwa sauti kama tulivyokuwa tukilia darasa la kwanza.
Baba wa taifa amefariki kwa hiyo taifa litakosa mzazi, tutaishije tukiwa mayatima? Hilo lilikuwa swali la kwanza kichwani mwangu niwa njiani kuelekea nyumbali palipokuwa si mbali na shuleni (kumbuka tulikuwa tukikaa nyumba za shule).Nilimkuta baba akiwa ameshika tama redio ikitoa sauti yake Sauti ya mamlaka ya Rais mkapa iliyokosa nguvu ilisikika kila baada ya dakika chache ikirudiwa kutangazwa kifo cha Mwalimu Nyerere.
Hapo nikagundua kilichomfanya baba awe mnyonge kwa karibu wiki mbili huku redio ikiwa ni rafiki yake mkubwa , mama naye alikuwa akielekea jikoni aliponiona pale sebuleni nikimtazama baba aliyelengwa na machozi ya uchungu, nikaamua kumfuata.
‘’Mama unamjua baba wa taifa?’’Nilimuuliza tulipofika jikoni.
‘’Ndiyo ni kiongozi wa kwanza wa Tanganyika huru, huyo ni mwanamapinduzi halisi , mjaa wa kweli masikini Mungu amemchukua kabla hajawasuluhisha warundi’’Mama aliongea kwa uchungu mkubwa maneno ambayo kwangu yalikuwa mageni sana.
‘’Baba yako ni mfuasi wa ujamaa wa kweli kama alivyokuwa Mwalimu na hayati Sokoine ndiyo maana akakuitwa Moringe anaamini utakuwa ni lama na ukumbusho kwake’’
‘’Sokoine naye amefariki?’’Niliuliza nikimfuta mama machozi.
‘’Ndiyo kwa ajali tata ya gari’’Aliongea mama kwa kifupi akianza kuhangaika na sufuria aandae chakula ambacho hata baada ya kuiva hakikuliwa na yeyote wote tulikuwa na hofu na uchungu mkubwa.
‘’Mapebari watakuwa wamefurahi, watauvinja na Muungano wetu kama walivyolizika azimio la Arusha mbele ya mcho yake’’ Nilimsikia baba akiongea kwa kifupi na kuingia chumbani.
Hivyo ndivyo kifo cha mwalimu kilivyopokelewa kwenye familia yetu, niambie  mlikipokeaje kwenu?

Kupata makala zaidi tembelea ukurasa wa Kalamu Yangu (Bofya hapa)

Juma Kaseja, tajiri anayedakia Mbeya City (Sehemu ya mwisho)


Na.Mwanakalamu
Katika sehemu iliyopita  tuliishia pale nilipopata taarifa za kutoka katika kile kijiji cha Kaseja mtoto lakini  kuna kitu nilichomwahidi yule mtoto na kumfanya afurahi sana.
Ni kitu gani hicho?  Tuendelee na simulizi hii ya kuvutia.
Baada ya kuzunguka huku na huko katika siku ile  iliyokuwa ya mwisho katika ziara yangu  nikiwa na yule rafiki yangu nilifanilkiwa kugundua mambo mengi sana.Katika niliyokuwa nimeyagundua ni majina ya wachezaji wachache sana wa Tanzania yaliyoikuwa yakisikia midomoni mwa  watoto lakini mwengi yalikuwa ni majina ya wachezaji wa Ulaya na Amerika.
Palikuwa na akina Messi, Rooney, Mata, Ronaldo na wengine wengi huku majina machache kama Kaseja, Mwameja,Tegete, Ngasa na mganda Okwi.Lakini kulikuwa na kitu cha ajabu kidogo kwani fualana nyingi za timu za nh’ambo zilikuwa na majina na namba za wachezaji wakati wale waliokuwa wamejiita majina ya wachezaji wa Tanzania walikuwa  ama wameaandika kwa rangi za nyumba ama wamechora kwa wino wa peni  au walikuwa hawajaandika chochote.
Ilinisikitisha sana, lakini sikuwa na namna zaidi ya kuamini kuna siku nitatumia kalamu kuufikisha ujumbe wangu kwa matajiri hao wakitanzania waliokuwa wakiziacha fedha zikiishia kwenye mitumba kutoka Ulaya iliyopitia Malawi na Msumbiji.
Siku iliyofuata nilisafiri kwa pikipiki hadi nilipofika kwenye mji ambapo palikuwa na gari zilizonifikisha Mjini Songea ambapo kitu cha kwanza nilichokifanya ni kutimiza ahadi yangu kwa Kaseja Mdogo.Niliingia kwenye duka moja la vifaa vya michezo ambapo nilipata kununua raba za michezo za saizi ndogo ,bukta na fulana nyekundu na nyepe kasha nikaingia mtaani kwa wataalamu wa nembo na michoro ya nguo ambapo niliwaeleza waaandioke namba moja na jina la Juma Kaseja Mgongoni.
Yule jamaa aliniangalia usoni na kuanza kufanya kazi niliyokuwa nimemweleza huku akionekana kutaka kuongea kitu lakini alionekana kama kuniogopa hivi.
‘’Vipi mbona kama kuna kitu unataka kuongea?’’ Niliamua kumuuliza.
‘’Hivi unajua Kaseja anachezea mbeya City?’’ Alinijibu kwa swali.
‘’Naaam nalijua hilo’’
‘’Mbona umemnunulia jezi ya Msimbazi?’’
‘’Kaseja ni Simba na Simba ni Kaseja’’Nilimjibu.
‘’Hiyo ilikuwa zamani  siyo leo’’Aliongea kama akinikosoa vile.
‘’Hapa hadi leo kaseja ni Simba sema Simba hawataki iwe hivyo,Masabiki tunatamani hata awe mshauri wa timu hata kama hachezi, iwe tuu kama Drogba alivyorudio pale chelesea ama anavyofanya Mgosi pale Msimbazi’’Nilieleza kwa masikitiko kidogo.
‘’Lakini si kwa viongozi wale , viongozi waliamua kumwacha kisa tuu yeye ni maarufu na tajiri kuliko wao’’Ananidokezea kitu huyun jamaa huku akionekana kuachana na ile kazi ya kuchora a,anaonekana mwenye hasira.
‘’Kwa hiyo Kaseja ni tajiri sana?’’ Namuuliza nikiwa siamini kauli yake.
‘’Ndiyo ni tajiri na anaweza kuwa tajiri zaidi’’
‘’Kivipi?’’
‘’Unaambiwa Kaseja ana miradi mingi kawekeza huko , lakini bado ananafasi ya kuwa tajiri’’Ananieleza yule jamaa wakati huu anaendelea kuchora.
‘’Kivipi?’’Nalirudia swali langu.
‘’Unajua hapa ulivyonunua hii jezi na kuja kuichora kwangu , hela hii ilikuwa yake ila hajaamua kuwekeza huku’’
‘’Ila kweli’’Najibun na kusubiri aongee inaonekana ana mengi sana.
‘’Unaona hii?’’ Ananiuliza akinionesha kitu kwenye simu yake.
Ni video iliyowekwa na Kaseja kwenye ukurasa wake wa instagram , inamwonesha akishuka kwenye basi huku akishangiliwa na kundi kubwa la watoto na vijana.Hapo ananikumbusha siku moja alipokuja na timu yake ya Simba  mwaka 2010 pale Njombe ambapo watoto wato walianza kumshangilia  tangu aliposhuka kwenye basi, pale hotelini walipolala wachezaji watoto walikuwa hawabanduki wakimchungulia Kaseja wakiita jina lake, kumbuka kipindi hicho Simba ilikuwa pia na akina Okwi sijui Mgosi lakini Kaseja alikuwa kivutio cha kila mtu.
Uwanjani pale Sabasaba ingawa hakuanza kucheza watoto walikuwa kwa kaseja tuu si kwa timu iliyokuwa uwanjani.
‘’Hiyo ilikuwa Shinyanga, kila apitapo hali inakuwa hivyo, Kaseja ana nyota ya akina Diamond, Lowasa na Alikiba’’Ananieleza yule jamaa baada ya kunionesha picha kadhaa za kaseja alizokuwa ameweka kwenya akaunti yake.
Lakini alinionesha picha moja ambayo iliniumiza moyo wangu ,ilikuwa ni picha iliyomwonesha akiwa uwanja wa Taifa akishangilia kipindi hicho yupo Simba, chini yake kuna maandishi.
‘’WANASIMBA MNIKUMBUKE KWA MABAYA YANGU’’
Hiyo ilikuwa pia ni komenti ya picha iliyokuwa imetangulia baada ya dada mmoja kumwambia anatamani arudi Msimbazi, huyo dada alidai kuwa amekuwa shabiki wa Simba kwa sababu yake hivyo hata haoni umuhimu wa kuwa  Simba, alkini Kaseja alimjibu huyo dada kuwa yeye na wanasimba wenzake wamkumbuke kwa mabaya yake.Iliumiza kweli kipenzi huyu wa Simba aliyaongea ya moyoni mwake , ilionesha wazi kuna kitu hakikuwa sawa katika kuondoka kwake msimbazi ingawa anaonekana kuwa na mapenzi mema na timu hiyo.
‘’Hii ndo Tanzania’’Niliongea kwa kifupi.
‘’Lakini ana nafasi’’ yule jamaa ananiambia kwa kifupi akiiweka vizuriile fulana ambayo alikuwa amemaliza kuichora.
‘’Kurudi Simba?’’Nauliza nikiwa nimehamaki.
‘’Hapana sahizi mkataba wake na Mbeye City umeshaisha tangu muda sasa, lakini aliamua kuitumikia timu hadi  mwisho wa msimu, anaweza kuongeza mkataba ama kwenda timu nyingine na hata akikosa timu anaweza kuendelea na soka akiwa kama mkufunzi ama mhamasishaji  wa wanasoka chipukizi.
 Makampuni yapo mengi awashawishi tuu wanaweka mpunga na kuanzisha kakituo kakizushi kanakuwa ni chuo cha kuwanoa makipa ambao watakuja kuisaidia nchi na hata kuuzwa nje, haijalishi hata kama yeye hatowafundisha yeye waletwe tuu wataalamu wamsaidie huku akizunguka nchi zima mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, tarafa kwa tarafa kata kwa kwata na kijiji kwa kijiji.
Hapo anaenda kutafuta wataalamu na wabunifu wanabuni jezi rangi na muundo wake zinaandiokwa jina lake, anaweka sokoni viatu , gloves na vifaa vingine vya michezo kasha anapozunguka kutafuta vipaji basi huko pia anaweka vituo vyake ambako vifaa vyake vitauzwa huko.
Nakwambia Kaseja ni tajiri mkubwa sana hata asipocheza soka, na katika soko ukiachana na bidhaa za urembo wa wanawake vitu vya watoto vinanunulika sana angalia hata we mwqenyewe umeamua kumnunulia mwanao nadhani baada ya kukusumbua, watoto wakiona watakulilia mzazi na kama nawe hueleweki mtoto anaweza kuiba akaipate jezi full ya Kaeja Tanzania One , Tajiri anayedakia Mbeya City’’.
Anamaliza yule jamaa akinikabidhi jezi zangu ambazo nziweka kwqenye mfuko na kwenda kumpa rafiki yangu mwenyeji wa kule kijiijini mwambao wa ziwa nikimwomba amfikishie rafiki yangu Kaseja mdogo.
Kuna kitu nakikumbuka , naamchelewesha tena yule mwenyeji wangu kwa kuingia palipo na huduma ya intaneti naishusha picha kadhaa za Juma Kaseja na kuzichapa kwenye karatasi naiweka kwenye bahasha na kwenda kuunganisha na ule mzigo wa jezi.
Ninaagana na rafiki yangu kasha naenda uwanja mdogo wa ndege na kufanya taratibu za safari na baada ya saa chache najikuta nipo kwenye jiji la joto , jiji lenye timu ambayo Kaseja ameitumia kwa muongo mzima.
Dah! Huyu ndiye Kaseja tajiri anayedakia Mbeya City.
Niandikie maoni yako hapa  chini.

Moyo mpweke (Nani nimuweke moyoni)


SHAIRI
Moyo wangu ni mpweke,kupendwa ninatamani,
Ila nimepigwa teke,hauna tena thamani,
Upo wapi njo udeke,usinombe samahani,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Asiwe kiruka njia,leo wangu kesho sina,
Aiweke yake nia,nami nimpende sana,
Akiona ninalia,anitake kupambana,
Nani nimweke moyoni, awe radhi myaka yote.

Tangu siku ninaachwa,na muhibu tunda langu,
Kutwa mi naachwa,silijui kosa langu,
Nilienda kichwakichwa,nitulize moyo wangu,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Si utani kweli tupu,moyo wangu u mpweke,
Siipendi tena supu,wala mahindi mateke,
Siyajui magrupu,nimeshakuwa mpweke,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Kila moja nina wangu,hakuna aliye singo,
Nikienda wanguwangu,naweza vunjwa mgongo,
Njia yangu sa ni chungu,nusu niivunje shingo,
Nani nimweke moyoni,awe nami myaka yote.

Nalala mimacho wazi,nausubiri ujumbe,
Mlango naacha wazi,mawazo we siombe,
Nikipigia wazazi,naiwaza hata pombe,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Hayupo kapata bwana,nabaki nayumbayumba,
Atamba bonge la bwana,tena aitwa mchumba,
Huyu naye ana bwana,wala siyo ombaomba,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Simu sasa nakatiwa,dakika zinabakia,
Eti mori wasumbuwa,mume ananipigia,
Pia kaa ukijuwa,mjanja katangulia,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Machozi yanizuia,kuandika ninalia,
Kama upo wasikia,njoo nitakupokea,
Cha msingi zingatia,napenda upende pia,
Niandikie nikujuwe,ukiona waweza penda.

Timu tano zinazoongoza kwa mauzo ya jezi duniani 2015/2016Mwaka huu umekuwa mzuri kwa timu ya Barca kwa mauzo mazuri ya jezi na kufikia jezi milioni 3,637 huku ikiziacha mbali kabisa Manchester na Real Madrid

Naamka tena concert. Tickets at OMGift Shop (Dar free market) na Shear Illusion(Mlimani City), Jackies Bar-Masaki na Samaki SamakiZimebaki siku sita tu kukinukisha pale Milimani City. Unasubiri nini kujipatia tiketi yako tarehe 20 Mei 2016, Naamka Tena Concert. Tiketi zimeanza kupatikana OMGift Shop - Dar Free Market, Shear Illusion - Mlimani City, Jackies Bar-Masaki na Samaki Samaki.
Kwa Wakazi wa Dar Es Salaam. 

Dodoma kaeni tayari tunakuja
Powered by EFm & East Africa TV/Radio

Maandalizi ya tamasha la Maji Maji Selebuka yazidi kupamba moto zikiwa zimebaki wiki mbili kuanza.

Maji maji Selebuka ni tamasha linaloandaliwa na Kampuni binafsi iitwayo Tanzania Mwandi ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Songea Mississippi (SO-MI). Shirika hili linahusika na mambo ya maendeleo ya jamii na elimu kwa wanaSongea kwa ushirikiano kati ya Songea Tanzania na Mississippi Marekani tangu lilipoanzishwa 2008.

Tamasha la Majimaji Selebuka 2016 linahusisha mambo yafuatayo;
 1. Mbio za nyika (Marathon)
 2. Mbio za baiskeli (Cycling)
 3. Ngoma za asili (Traditional Dances)
 4. Mdahalo wa shule za sekondari (Schools debate)
 5. Maonyesho ya ujasiliamali na biashara (Trade fair and entreprenuership)
 6. Utalii wa ndani (Local tourism)
Mwaka huu tamasha la Majimaji Selebuka litafanyika kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 04 Juni 2016 katika viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa vita vya majimaji mjini Songea katika mkoa wa Ruvuma Tanzania.

Tamasha hili linafanywa kwa lengo la:
 1. Kuibua vipaji na kuviendeleza kupitia michuano ya kimichezo. Kutakuwa na mashindano ya Mbio za Nyika(Marathon) 42km, 21km, 10km na 5km(Run for fun), na Mbio za baiskeli ambazo tunaamini kwa mwaka huu zitakuwa za aina yake kwa sababu tunategemea kupata washiriki wa mbio za baiskeli kutoka nchi za jirani kama Rwanda.
 2. Kuibua na kutambua fursa za kiuchumi hasa kwa wajasiriamali wa mkoa wa Ruvuma kupitia maonyesho ya shughuli za wajasiriamali pamoja na biashara katika viwanja vya Makumbusho ya vita vya majimaji kwa siku saba mfululizo kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 04 Juni 2016. Lengo likiwa ni kupanua soko la wajasiriamali kwa watu tofauti kwani kutakuwa na wageni mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi.
 3. Tamasha pia linalenga kuiendeleza elimu kupitia midahalo wa shule za sekondari.Katika kipengele hiki wanafunzi kutoka shule mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma, watapata nafasi ya kuchuana katika mdahalo ulioandaliwa na waratibu wa tamasha hili la Majimaji Selebuka. Mdahalo utafanyika tarehe 01 mpaka tarehe 02 Juni, 2016.
 4. Pia tamasha linalenga kuibua fursa za kiutalii zanazopatikana mko wa Ruvuma kupitia Utalii wa ndani.
Tutaanza tamasha kwa Mbio za Nyika (Marathon) ambazo zitafanyika siku ya ufunguzi tarehe 28 Mei 2016 kuanzia saa 12 asubuhi. Na tutafunga dimba kwa Mbio za baiskeli siku ya kilele cha tamasha la Majimaji Selebuka tarehe 04 Juni 2016. Ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha hivyo watu wasiwe na wasiwasi juu ya hilo.

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi watakaoshiriki katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2016. Kama vile Medali, Vikombe, Ngao, Vyeti,Fedha taslimu pamoja na zawadi nyingine kutoka kwa wadhamini wa kila tukio. Lakini pia kwa washindi watatu wa mbio za baiskeli watapata nafasi ya kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya mafunzo ya mbio za baiskeli za kimataifa.

Kwa sasa fomu za ushiriki zinapatikana kwenye tovuti yetu ambayo niwww.somi.international kwenye kipengere cha ‘DOWNLOADS’ hivyo basi kila mtu popote alipo anaweza kuingia na kuzichukua mda wowote anaotaka yeye.
Ada ya kushiriki katika tamasha itakuwa kama ifuatavyo;
 • Mbio za Nyika (Marathon); 42km – 10000/=, 21km – 5000/=, 10km – 3000/= na 5km(Run for fun) - Bure
 • Mbio za baiskeli; 50km – 10000/=
 • Ngoma za asili; kila kikundi – 10000/=
 • Maonyesho ya ujasiliamali; Kikundi – 50000/=, Mtu mmojammoja – 10000/=

Kwa maelezo zaidi tafadhari tembelea website zifuatazo;
Songea Mississippi; www.somi.international
Tanzania Mwandi; www.tanzaniamwandi.com


Imeandaliwa na;
Reinafrida M Rwezaura
Mratibu wa tamasha la Majimaji Selebuka

Most Read

Translate

Follow by Email

Followers

Pageviews

Google+ Followers