Nyota wa zamani wa Liverpool na Cameroon Rigobert Song hatimaye amezinduka baada ya kuzimia kwa siku mbili mfululizo. Daktari wa Hospital ya mjini Yaounde amesema kuwa mlinzi huyo atasafiri kuelekea Ufaransa kuendelea na matibabu zaidi. Song mwenye miaka 40 aliripotiwa kuzimia akiwa nyumbani kwake siku ya jumapili.
BBC wameripoti kuwa daktari mkuu wa Yaounde Hospital Central Emergency Centre Louis Joss Bitang A Mafok amesema Song ameondolewa kifaa maalum cha kupumualia na tayari anapumua kawaida. Song anashikilia rekodi ya kucheza michezo 137 kwenye timu yake ya taifa pamoja na kucheza fainali nne za kombe la dunia huku AFCON akiwa amecheza fainali nane.
0 comments: