Faith Chepgetich Kipyegon wa Kenya siku ya Jumanne alishinda mbio za mita 1500 za wanawake na kuipa Kenya medali ya tatu ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Rio 2016.
Kipyegon alimtoka bingwa wa dunia Genzebe Dibaba wa Ethiopia katika dakika za mwisho na kumaliza mbio hizo katika muda wa dakika 4, sekunde 08.92 wakati Dibaba alichukua medali ya fedha katika muda wa dakika 4, sekunde 10.27
Jennifer Simpson wa Marekani alichukua medali ya shaba katika nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 4, sekundu 10.53
Ushindi wa Kipyegon umeifanya Kenya kupata medali ya dhahabu kila siku kuanzia Jumapili na mpaka sasa ina medali tatu za dhahabu na tatu za fedha na kuongoza bara la Afrika ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye medali moja ya dhahabu, nne za fedha na moja ya shaba
0 comments: