Kwa utafiti mfupi na wa haraka nimegundua nchi ambazo raia wake ni wachapakazi ndizo zenye maendeleo makubwa duniani. Hivyo nikakumbuka ile tafiti ya watu, sikumbuki taasisi gani waliyofanya wakasema katika Afrika mashariki Watanzania ndio huongoza kwa matumizi ya mitandao ya kijamii. Ndipo nikafanya connection kati ya maendeleo na mitandao ya kijamii na kuwaza labda Tanzania hatuna maendeleo makubwa kwa sababu ya matumizi makubwa na hasi ya mitandao ya kijamii inayopelekea kusifanyike kazi za kimaendeleo ipasavyo.
Nikawa natafuta mfano mahususi na kupata mfano ambao unathibitisha hilo. Mfano niliyoichukua ni katika kundi moja la WhatsApp nililoachana nalo baada ya kukaa kwa muda wa wiki mbili tu. Kwanza niliona ajabu sana siku za kazi (Jumatatu - Ijumaa) watu wako bize kuchati mambo yasiyokuwa na maana na wanachangamka kweli kweli. Lakini siku za wikendi walikuwa kimya kabisa, ndipo nikajithibitishia kuwa laiti kama ule muda mrefu wa kuchati ungekuwa unatumika ipasavyo kwenye kazi ninauhakika uzalishaji mali na huduma ungekuwa mkubwa sana katika sekta zote yaani binafsi na serikalini. Pia kungekuwa na ufanisi mkubwa sana katika kazi kwani muda wa kazi watu wangefanya kazi kwa umakini zaidi na muda wa mapumziko baada ya kazi na siku za wikendi zingetumika kuchati.
NB: Time management is a vital factor for sustainable Development
0 comments: