Ukitaka kuwa mbaya dai chako. Mjini shule!

on Wednesday, August 31, 2016 - No comments:

Image result for women shocked at husband cheating
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.
Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!
Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp...!
_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._
--
_*Kisha nikaituma ile message*_
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake... Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.
*Akatuma message akiniuliza...*
_Hao wanawake unawajuwa, ...mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli...!_
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa...!
Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa...! Akaniandikia message nyingine....
*...Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe... Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri...!*
Nami nikamjibu...
_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo...!_
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai...!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa.... Kama sio mie!

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends