Kama unakumbuka kwa muda sasa maeneo ya kariakoo yamekuwa hayana wamachinga katika maeneo ya barabara na kuacha njia nyingi kuwa wazi. Lakini kufuatia tamko la Mh. Raisi wamachinga hao wamerejea kwa kasi kubwa za mitaa ya kariakoo pembezoni mwa barabara huku suala hilo likiwa limefurahiwa na asiilimia kubwa ya wamachinga hao. Lakini kwa upande mwingine baadhi ya watu imeonekana ni kero kwao hasa wamiliki wa maduka kwani wanasema kuwa wamachinga hao wamekuwa wakiuza vitu hivyo kwa bei ya chini na kusababisha wateja kukimbilia kwao. Pia wengine wamelalamikia suala hilo kwani wamachinga hao wamekuwa wakileta shida katika maeneo ya barabara kwa kupanga vitu hadi maeneo ya barabara.
Kufuatia suala hilo Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametoa tamko kuhusiana na suala hilo. Msikilize hapo chini.
0 comments: