Cameroon forward Samuel Nlend
Siku chache baada ya kusaini dili la kuichezea klabu ya Al Ittihad ya nchini Misri, Samuel Nlend (Miaka 21) amejikuta katika wakati mgumu baada ya mkataba wake kusitishwa kutokana na kukutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Habari hizo ziliripotiwa na chombo cha habari kutoka Misri, KingFut.com kuwa taaria hiyo ilitolewa na msemaji wa klabu hiyo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.
Hakuna sheria inayomkataza mtu kujishughulisha na masuala ya soka lakini Nlend hatoweza kupata nafasi ya kufanya kazi katika nchi nyingine kutokana na hali yake ya afya, aliongeza.
Nini maoni na matazamo wako juu ya suala hili?
Usisite kuacha maoni yako hapa chini na tutayajibu.
0 comments: