Kituo cha watoto waishio katika mazingira hatarishi cha Nico Polic Academy chawatembelea wagonjwa.

on Wednesday, August 31, 2016 - No comments:

 uongozi wa kituo cha NICOPOLIC ACADEMY ukiwa na watoto wa kituo hicho wakitoa msaada wa watoto wenzao ambao ni wagonjwa katika hospitari ya wilaya ya Ludewa

 Kaimu mganga mkuu wa hospitari ya wilaya ya Ludewa Dkt.Frank Mwambasanga
Wodi ya watoto katika hospitari ya wilaya ya Ludewa 


Kituo cha watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimetoa misaada mbalimbali kwa watoto wenzao ambao ni wagonjwa na wamelazwa katika wodi ya watoto hospitari ya wilaya ya Ludewa.

Akitoa msaada wa Sabuni na vitu vingine jana  kwa watoto waliolazwa katika hospitali hiyo Mkurugenzi wa NICO POLIC ACADEMY Bw. Augustino Mwinuka alisema kuwa lengo la kwenda na watoto wa kituo hicho ili kuwajulia hali watoto wagonjwa waliolazwa katika hospitari ya wilaya ya Ludewa ni kuwafundisha watoto wa NICO POLIS ACADEMY kuwa na matendo ya huruma.

Bw. Mwinuka alisema kuwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanatakiwa kujifunza upendo kwa kuonesha watoto wengine hivyo ni utaratibu wa kituo hicho kuwatembeza watoto hao katika kuisaidia jamii nyingine yenye shida zaidi ya watoto wanaotoka NICOPOLIS ACADEMY.

Alisema kuwa kituo hicho kinachukua watoto wa aina mbalimbali ambao ni watoto wenye ulemavu wangozi,watoto yatima na wanaoishi mazingira hatarishi pia baadhi ya wazazi huwaleta watoto wao ili waweze kupata elimu kwa kuchangia gharama nafuu.

“Tumewaleta watoto hawa kuwaona watoto wenzao ambao ni wagonjwa na kuwapatia vitu vichache ili kuwafundisha watoto tulionao katika kituo chetu waweze kuwa na moyo wa huruma na kuwajali wengine kwani watoto wengine tulio nao wameharibiwa kisaikolojia kutokana na maisha waliokuwa wakiishi kabla ya kuja kuishi katika kituo chetu hivyo inaweza kusaidia kuwaweka sawa katika jamii”,alisema Bw.Mwinuka.

Akitoa shukrani zake kwa uongozi wa kituo cha NICO POLIC ACADEMY kaimu mganga mkuu wa Hospitari ya wilaya ya Ludewa Daktari. Frank Mwambasanga alisema kuwa kituo hicho ni mfano wakuigwa kwani wameonesha kuwa wapo kwaajili ya jamii na si vinginevyo.

Dkt.Mwambasanga alisema kuwa kituo hicho kimetoa faraja kwa watoto hao ambao ni wagonjwa richa ya kuwa wamekuja kuwafundisha watoto wanaoishi kituoni hapo kushiriki katika shughuri za kijamii lakini kwa misaada yao na zawadi walizowabebea watoto wenzao nifaraja kubwa kwa wauguzi wao na wagonjwa kwa ujumla.

Aidha Dkt. Mwambasanga aliwataka wadau na viongozi wa shule mbalimbali wilayani hapa kuiga mfano wa kituo hicho ambacho kinatambua umuhimu wa kuwatembelea wagonjwa kwani kwa kufanya hivyo wagonjwa watafarijika kutokana na hali halisi kuwa shule za wilaya ya Ludewa hazina utamaduni wa kuwatembelea wagonjwa.


Mwisho.

Tagged as: ,
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends