Michoro ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo kijijini Kwembe katikati ya Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam. Hii ni sehemu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) inayojengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa mwaka, na pia itakua sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini. Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, ujenzi wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake imeshapatikana, unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi kuanza. Kwa maneno mengine Kampasi ya Muhimbili ya Mloganzila inategemewa kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka 2015. Tayari wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya Mloganzila wameshaanza mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600). Sambamba na kampasi ya MUHAS ya Mloganzila pia ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umeshaanza na kufikia hatua ya juu na ambapo pia hospitali hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba mchakato wa kufanikisha uanzishaji wa Chuo Hospitali hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na mafunzo mbalimbali. Chuo hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa, ikiwa ni mikakati kabambe ya serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi ina wataalamu wengi na huduma za kisasa za afya ili kuondokana na adha ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Kwa sasa MUHAS inachukua takriban wanafunzi 2442 wa udaktari na huduma za afya kwa mwaka. Hivyo ujio wa kampasi ya Afya Mloganzila na Kampasi ya afya ya UDOM utaharakisha mpango wa serikali wa kupunguza wastani wa wagonjwa kwa daktari mmoja kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa wastani ni daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000.
Habari, Michezo, Siasa, Elimu, Muziki na Matangazo
You are here: Home
» MICHORO YA CHUO CHA MUHIMBILI KINACHOJENGWA MLOGANZILA KISARAWE
MICHORO YA CHUO CHA MUHIMBILI KINACHOJENGWA MLOGANZILA KISARAWE
on Monday, November 26, 2012
-
No comments:
Tagged as:
About Unknown
“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Share This Post
Related posts
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Like, share and send to friends
KARIBU
Popular Posts
-
KUWENI NA SUBIRA WADAU WETU TCU WAMEIONDOA ILE SELECTION STATUS FUATA HATUA HIZI ILI KUWEZA KUONA CHUO ULICHOCHAGULIWA Ingia kwenye website...
-
KUPATA MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2015 BOFYA HAPA... (2015 RESULTS CLICK HERE) NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2013 E...
-
CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHATANGAZA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO HICHO KATIKA FANI MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013 The...
-
Kupata matokeo ya kidato cha nne 2013 BOFYA HAPA Kupata matokeo ya QT 2013 BOFYA HAPA MATOKEO CSEE 2013 ...
-
S4567 SACRED HEART S4568 ROYAL S4569 ST MARIE EUGENIE S4570 MAGUNGU S4571 KIJUNGU S4572 IPWAGA S4573 UWANJA WA TAIFA S4574 ITONA S4575 MESSA...
-
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015 BOFYA HAPA Kupata matokeo hayo bofya hapo chini MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 (NATIONAL FORM FOUR RESUL...
-
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI MWAKA WA MASOMO 2012/2013 MAELEK...
-
Bofya hapa kuangalia matokeo ya darasa la saba Waweza pia kuchagua mkoa unaotaka kwa kubofya kwenye mkoa husika ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA ...
-
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, anawatangazia vijana wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2...
-
The following candidates have been selected to join LGTI for the academic year 2013/2014 which starts on Saturday, the 24th of ...
0 comments: