IVA YOUTH GROUP LUDEWA WAANZA KUTENGENEZA FILAMU

on Monday, February 24, 2014 - No comments:


Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi 
 Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi 

 Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi 
Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi

Kikundi cha sanaa kijulikanacho kwa jina la IVA YOUTH GROUP kilichoko wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeanza kutengeneza Filamu yao ambayo inamahadhi ya wilaya ya Ludewa ikiwa ni Filamu ya kwanza tokea wilaya hiyo innzishwe.

Akiongea na wanahabari wakati wa kurekodi Filamu hiyo katibu wa kikunchi hicho Bw.Leonard Lukuwi alisema IVA YOUTH GROUP ni kikundi pekee kilichosajiriwa na baraza la sanaa la Taifa(BASATA) kunafanya kazi mbalimbali za uelimishaji wa jamii katika wilaya ya Ludewa na knapatikana Ludewa mjini

Bw.Lukuwi alisema kuwa kikundi hicho kimekusanya wasanii mbalimbali katika kata na vijiji vya wilaya ya Ludewa na kufikia wasanii 30 ambao wanafanya sanaa mbalimbali na mpaka sasa wanaandaa Filamu ya kwanza ambayo itawatambulisha wanaludewa na tamaduni zao.

Alisema kuwa wilaya ya Ludewa inawasanii wenye vipaji vikubwa lakini wamesahaulika kutokana na kukosa wadau ambao wangeweza kuwaibua na kuitangaza wilaya yao katika Taifa na mataifa mengine ambayo yanafuatilia sanaa za Tanzania.

“vipaji vipo Ludewa ila kinachokosekana na ufadhiri kwani mpaka sasa kikundi cha IVA hakina mfadhiri na hakija wahi kupata ufadhiri wa aina yoyote licha ya kuwa ni kikundi kikongwe kilianzishwa mwaka 2008 lakini kimekuwa kikitumiwa na mashirika katika kuielimisha jamii katika mambo mbalimbali na sasa tumeamua kutengeneza filamu hii kwa kujichangisha wasanii wenyewe ili tuweze kuinua uchumi wetu ndani ya kundi”,alisema Bw.Lukuwi.

Filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa mwezi juni mwaka huu ikiwa na wasasii chipukizi ambao kwa mara ya kwanza wataanza kuonekana katika ulimwengu wa Filamu nchini hivyo amewaomba wadau mbalimbali kutoa michango kwa njia ya mpesa katika namba 0752 206242 ili kufanikisha filamu hiyo.

Tagged as:
Goodluck Mshairi About Goodluck Mshairi

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends