ZITO KABWE AELEZA KWA KIFUPI HISTORIA YA MAMA YAKE WAKATI WA KUAAGA TAYARI KWA SAFARI YA KIGOMA

on Sunday, June 1, 2014 - No comments:

Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri). Ameacha mume, na watoto 10, wanaume 6 na wakike wanne. alisema Zitto.

Mama yake Zitto, alifariki mapema saa 5 asubuhi, akiwa na umri wa miaka 64, kwenye hospitali ya AMI, Msasani jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya kizazi baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu.


nyumba ya mapumziko ya milele.
============================== ============================== =====


Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza kwenye gari jeneza lenye mwili wa Saida Salum, mama mzazi wa Zitto tayari kuelekea uwanja wa ndege.



Wakazi wa jiji wakiingiza mwili wa Mama mzazi wa Zito Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Shida Salumu)katika gari tayari kwa Safari ya kuelekea Kigoma mara baada ya kuswaliwa katika msikiti wa Maamul jijini Dar es Salaam jana.Marehemu anatarajiwa kuzikwa mjini kigoma

Mbunge wa Musuma Vijijini Nimrod Mkono (kulia) na Mbunge wa Bunda Stephen Wasira (kushoto) wakifariji Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zito Kabwe kwa kufiwa na Mama yake Mzazi.


Picha chini zinaonyesha baadhi ya waombolezaji waliohudhuria swala ya kuswalia Marehemu Shida Salum, Mama yake Zitto Kabwe.





Zitto kabwe akiwa na Prof Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi.

Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe.

Kardinali Polycarp Pengo akiwa na Rais wa TASWA, Juma Pinto akiwa VIP JKN Airport walipokutana wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe,

Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe, Bi Shida Salum kuingiza kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi

Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na mwezie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends