EXCLUSIVE : HAMISA MOBETO KUVISHWA PETE YA UCHUMBA TAREHE 2 YA MWEZI WA 8 NDANI ESCAPE 1.

on Tuesday, July 29, 2014 - No comments:

Wanasema kimya kingi kina mshondo baada ya kudaiwa, hapo mwanzo ilidaiwa kua  Hamisa Mobeto alikua akichepuka na Bwana Almas aka Dangote aka Diamond au Chibu kama mwenyewe anavyopenda kujiita. Lakini baada ikaja kujulikana kua yalikua ni maneno ya wabongo.
Habari za kuaminika Bongoclan ilizozipata ni kua kwa sasa Mwanadada Hamisa kazama kabisa kwenye penzi zito la Seth De Jesus Giovan almaarufu kama Bikira wa kisukuma. Mmoja wa mashostito wa wapenzi hao ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kua Hamisa keshatambulishwa nyumbani kwao na Bikira na kilichobaki ni tukio la kuvishana pete ndo lililobakia.
Team yetu iliamua kufatilia kama ni kuna ukweli  kuhusiana na ishu ya kuvishana pete kwa wapenzi hao na kugundua ni kweli kua watavishana pete tarehe 2 ya mwezi wa 8 ndani ya Escape 1 ambako pia ndani ya siku hiyo kutakua na Instagram Party.


Kupitia akaunti yake bikira wa kisukuma alifunguka haya kuhusiana na tukio hilo " Mungu anipe nini mie...Nimeokota Embe Dodo vhini ya Mpera..I cant wait tarehe 2 pale ESCAPE 1.. Asante Mungu kwa kuileta INSTAGRAM maana nisingempata huyu na kudolishia watu hapa... Nakupenda we mtoto kuliko Ng'ombe anavyopenda majani,Nakuhusudu kuliko Mngoni anavyopenda ngono,Nakuthamini kama Mchungaji anavyoithamini Biblia... I cant wait to engage you pale jukwaani mbele ya halaiki maelfu TAREHE 2...Kama Chibu kaweza kwanini mie nishindwe...Niko tayari kuwa bwege juu yako hamisa wangu,Sitakuwa na wivu wala SitakuSPY kama mme wa yule dada nanii yule mtangazaji,Msukuma nimezama kwako @hamisamobeto DONT MISS MY ENGAGEMENT PARTY kwenye INSTAGRAM PARTY TAREHE 2...iam excited..Nikipigwa kibuti ntalia balaa ntafunga akaunti wallah"
 
Pia inadaiwa kua Hamisa amewaalika mastar mbalimbali ambao watahudhuria tukio hilo wakiwemo Diamond akisindikizwa na Wema,  Adam Mchomvu, William Malecela, Jerry Slaa na wengine kibao huku burudani ikitolewa na Skylight Band.
Kiingilio siku hiyo itakua ni elfu 10 tu huku mambo yakianza mapema kuanzia saa1 ya usiku.
Unakaribishwa Kusoma habari za udaku na za siasa kila siku, usikubali kupitwa, like page yetu ya swahilitz katika facebook na pia usisahau kutufollow katika instagra @swahilitz vile vile katika twitter @swahilitz1.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends