SABABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA KISUKAZI

on Friday, May 29, 2015 - No comments:



Tunasisitizwa sana kufanya mazoezi kwa takriban nusu saa kwa siku na ambayo mtu anatoa jasho na moyo kumwenda mbio. Hiyo ni kwa ajili ya kusaidia misuli ya miguu, tumbo, kifua, mgongo na mikono kutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini. Kadhalika, wataalamu wanasisitiza sana kula vyakula visivyokobolewa, ikiwamo kula dona badala ya sembe, ulezi, mtama na matunda. Watu wapunguze na ikiwezekana kuacha kunywa vimiminika vyenye sukari, ikiwamo juice, soda, pombe na vinginevyo. Na hiyo ni kwasababu vinywaji hivyo havikai tumboni na badala yake huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida. Vyakula visivyokobolewa vina faida sana kwani vinachukkisukari - itete hospitalua muda wa kutosha kutoka kwenye tumbo na kwenda kwenye utumbo mwembamba hatimaye kuvunjwavunjwa kwa ajili ya kutumika mwilini.
Kadhalika makapi yatokanayo na hivyo vyakula hutuzuia kupata kansa ya utumbo. La ajabu wametoa takwimu za kutisha kwani ulaya kwasababu wanakula vyakula vilivyokobolewa wanapata kansa ya utumbo kuliko nchi au bara la afrika, na kansa hiyo ni ya nne kwa kusababisha vifo barani ulaya na amerika.
Tafadhalini, tujihadhari kwa afya zetu; mazoezi ni muhimu, vyakula viwe na uasilia wake, mtu aliye na mwenza wake afanye tendo la ndoa kwa kadiri inavyowezekana kwani ni sehemu ya mazoezi, tubadili mifumo ya maisha yetu na kukaa tu bila kujishughulisha mili yetu.
Tunawatakia wiki njema na afya njema.
JIHADHARI! KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends