MH. ZITTO KABWE ATOA YA MOYONI KUTOKANA NA KUUNGUA KWA SOKO LA MASASI

on Thursday, June 25, 2015 - No comments:

Baada ya kutembelea soko hilo lililoungua Mh. Zitto alikuwa na haya ya kusema kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
 
Soko la Masasi limeteketea. Licha ya wananchi kulipa tozo ya Zimamoto hapakuwa na msaada wowote kwa masaa zaidi ya 15 ambayo moto umeteketeza kila kitu. Wafanyabiashara hawa wamerudishwa kwenye ufukara. Hapa ndio tunaona umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa mujibu wa Azimio la Tabora la chama cha ACT Wazalendo. Wafanyabiashara hawa wangekuwa na hifadhi ya jamii kungekuwa na Fao la Majanga na hivyo wangerejeshwa kwenye hali yao ya kabla ya ajali. Hata hivyo, kama ajali hii ni hitilafu ya umeme lazima Shirika la TANESCO lilipe fidia kwa wananchi. Tumefikishwa mahala ambapo janga moja tu kama hili laweza kumrudisha raia kwenye dimbwi la umasikini. Lazima tubadilike.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends