Octoba 15, 2015 taarifa ya Majonzi ilitufikia ambapo taarifa yenyewe ilikuwa inahusu msiba wa watu wanne wakiwemo Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe na aliyekuwa Baba mzazi wa meya wa Ilala, William Silaa baada ya kupata ajali kwenye helikopta iliyoanguka katika msitu wa mbuga ya Wanyama ya Selous.
Taarifa kuhusu Ratiba ya kuwasili kwa miili hiyo Dar es Salaam na shughuli za kuaga miili hiyo pamoja na Ratiba ya Mazishi tayari ilitolewa, ambapo leo Octoba 17, 2015 marehemu Deo Haule Filikunjombe pamoja na wengineo waliofariki kwenye ajali hiyo ya helikopta waliagwa Mbagala Dar es Salaam kuelekea Ludewa mkoani Njombe kwaajili ya mazishi.
0 comments: