Hizi ndizo kazi ambazo unaweza pata wanawake wa kuoa kibongo bongo

on Monday, January 4, 2016 - No comments:


  • Mawakala wa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel money: Hebu jaribu kupata picha kila siku wakala wa huduma ya pesa kwenye simu anaandika namba ngapi za simu anapowapa huduma hiyo? Lakini katu huwezi kuta wakiwapigia simu kuwataka kimapenzi au kwa ajili ya kuanzisha mahusiano nao kitu ambacho ni toffauti na pale wakala anapokuwa wa jinsia ya kiume.
  • Walimu: Mwalimu ni mtu muhimu sana katika jamii kwani ndio mlezi wa pili wa mtoto kwani ndie ambae hukaa na watoto wetu kwa muda mwingi zaidi kuliko hata mzazi husika wa mtoto. Hebu fikiria ni mangapi ambayo yanamkuta akiwa na mtoto wako? Lakini ni mara chache sana hatokuwa mwaminifu katika kuhakishisha mtoto wako anapata elimu na malezi bora.
  • Manesi:  Pia umuhimu wake katika jamii kila mtu anafahamu, nadhani unaweza ukawa shahidi yangu katika hili kama umeshawahi kukutana na ugonjwa na ukafikisha hospitali kwa jinsi ulivyopokelewa kama anakufahamu au ni ndugu yako wa damu na kuhakikisha unapata huduma salama. Siku zote wamekuwa ni wapole na watu wenye kufanya kazi yao katika uadilifu mkubwa.
  • Wahasibu: Mhasibu ni mtu anayetunza pesa katika taasisi fulani au kikundi fulani. Watu hawa wanauwezo mkubwa sana wa kuhakikisha kile kilichopangwa kutumika ndicho kinatumika kufuatia bajeti husika. Kama wakuwa na uwezo wa kuweka usawa mahsusi katika mambo ya fedha basi naamini hata katika familia watakuwa na uwezo huo wa kuhakikisha kuwa familia inakuwa katika hali ya usawa
  • Wapishi hotelini/mgahawa: Ni mara ngapi umeweza hudhuria maeneo mbalimbali ambako chakula huuzwa. Je kunautofauti gani na pale unapokula nyumbani? Ikatokea ukamuuliza  mtu kuhusiana na chakula kizuri au kitamu ambacho amewahi kula lazima atarejea katika hoteli ambayo amewahi kula na si nyumbani labda kwa mke wake au binti yake wa kazi, atakuambia ni kile alichowahi kula mgahawani/hotelini
Nadhani utakubaliana nami juu ya ukweli huu kuhusiana na wanawake wakuoa. Endelea kutufuatilia Mwanaharakati Mzalendo kwa  habari zaidi

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends