NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA

on Tuesday, January 26, 2016 - No comments:

 
 1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote. 
 2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa. 
 3. Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema. 
 4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote. 
 5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu. 
 6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu hasiye sahihi. 
 7. Aina tatu za wanaume/Wanawake wa kuepukwa:a) Walevi. b) Malaya. c)Wagomvi.
 8. Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha. 
 9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa: a) Nakupenda. b) Samahani. c) Asante. 
 10. Kupiga punyeto ni kujiharibu. 
 11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga bila jua. 
 12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu: Mungu mmoja - Mume mmoja - Mke mmoja. 
 13. Furaha ya kudumu maisha hutegemea na chaguo lako la Ndoa. 
 14. Usioe pesa au mali - muoe mtu. 
 15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani na furaha. 
 16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa. 
 17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa kigezo tu anakidhi haja zako kingono. 
 18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. 
 19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali. 
Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza.
Nawatakia Siku njema ndugu/jamaa na marafiki wote

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends