The Industry label inayomilikiw na wanamuziki Nahreel na Aika kumsajili msanii mpya wa Rap

on Friday, January 15, 2016 - No comments:

THE INDUSTRY MUSIC LABEL

TAARIFA KWA UMMA
UTAMBULISHO WA MWANAMUZIKI MPYA WA STUDIO YA MUZIKI YA “THE INDUSTRY”
Uongozi wa Studio ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Wanamuziki Producer Nahreel na Aika Marealle unapenda kuchukua Nafasi hii kuwatangazia Umma Kuwa kuanzia Tarehe 14 January 2016 Wamemuingiza Msanii mpya wa Kike aitwaye Rosa Ree, Rose Ree ni muimbaji wa Muziki aina ya Rap ambae kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi kuanzia sasa katika Redio Mbali mbali na TV Stations za Tanzania na nje ya nchi.
Kama wasikilizaji na watazamani tunaomba Kumuunga mkono Msanii huyu mpya Kwani tuna uhakika hatawaangusha katika kuwaletea burudani Katika Masikio na macho yenu pindi kazi zake zitakapoanza kutolewa hivi karibuni.
The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle
Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake kama Don’t Bother na nusu nusu.
Instagram: @rosa_ree
Imetolewa na,
The Industry PR
John Kiandika

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends