Alex Morgan, mwanasoka wa kike mwenye wafuasi wengi zaidi katika mitandao ya kijamii duniani

on Saturday, April 9, 2016 - No comments:




Social Media
 2,667,696 Fans
 44,584 Talking About This
 2,213,543 Followers
 82.6 Klout Score


Alexandra Patricia "Alex" Morgan (Kuzaliwa, Julai 2, 1989)  ni mwanasoka Mmarekani kutoka Diamond Bar, iliyoko katika jiji la California. Ni mmoja ya wachezaji wakubwa aliyebobea katika mambo ya soka na mwanachama wa timu ya soka ya wanawake, Marekani.
Morgan alikuwa ni mwanasoka mwenye umri mdogo zaidi katika timu ya taifa katika kikoso cha timu ya taifa ya wanawake iliyoshiriki kombe la dunia la wanawake mwaka 2011.
Umuhimu mkubwa wa Morgan ulionekana pale ambapo aliiwezesha timu yake ya taifa ya wanawake kuchukua ushindi katika kufuzu kucheza kombe la dunia la mwaka 2011, huko Ujerumani na kuifanikishia timu yake kuchukua medali ya shaba katika michuano hiyo mikubwa kabisa ya soka duniani. Pia kufanikiwa kushiriki katika michuano ya Olympic, London.
Baadae mwaka 2012, aliiwezesha timu yake kutoka kidedea katika michuano ya Olympic na kutwaa medani za dhahabu.
Alex Morgan akipambana vikali na Saki Kumagai wa Japani katika moja ya mechi ambayo Marekani ilitoka na ubingwa na kutwaa medali ya dhahabu
Alex amefanikiwa kuchukua tuzo ya mwanasoka wa kike wa mwaka 2012 nchini marekani (2012 U.S. Soccer Female Player) na mwanasoka bora wa mwaka wa dunia, tuzo iliyotolewa na FIFA (FIFA Player of the Year).

Nje na soka Alex akishirikiana na Simon na Schuster wamefanikiwa kuandika kitabu kilichoongoza kwa mauzo na kushika namba saba kwa mauzo kilichoitwa "The Kicks" mwaka 2013, na kufuatiwa na maandiko mengine kama "Sabotage season" , kilichotoka mwaka 2013 pia.
Moja ya kitabu kilichoandikwa na Alex Morgan
Imeandaliwa na Mr. Kaozat (kaozat1@gmail.com | 0655 987 588)

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends