Usichokijua kuhusu milima

on Thursday, April 14, 2016 - No comments:


Na.Steven Mwakyusa

Ukiitazama sura ya dunia hasa nchi kavu utakutana na milima na mabonde, ipo milima ya aina mbalimbali kutokana na namna ilivyofanyika mpaka kufikia hapo ilipo!! Milima ni miinuko ambayo ina urefu kuanzia mita 600 toka usawa wa bahari!
#1 Milima iliyopo pwani ya Norway, Brazili, Australia, magharibi mwa India na kwingineko inakadiriwa kuwa na umri wa miaka 1000 mpaka 1200 million!
#2 Kuna aina kuu tatu za milima, milima ya volcano(volcanic mountains), milimamikunjo(fold mountains) na milima tofali(block mountains). 
#3 Mlima Everest ndiyo mlima mrefu zaidi katika uso wa dunia kwa maana ya nchi kavu ukiwa na futi 29,028.Mlima Everest unapatikana katika mpaka wa Nepal na Tibet barani Asia!
#4 Mlima Kilimanjaro ni wa 10 kwa urefu duniani ukiwa na futi 19,317.
#5 Milima imekuwa chanzo cha kufanyika mvua kwa kulazimisha upepo wenye mvuke kupanda juu na baadaye kusababisha mvua nyingi katika upande unaopakana na bahari (Windward side), huku upande wa pili ( Leeward side ukipata mvua chache au kukosa kabisa.
#6 Safu ndefu zaidi za milima katika nchi kavu ni milima ya Andes yenye urefu unaofikia 7200 km, katika safu ndefu zaidi ni zile za Mid-Antlantic ridge zenye urefu wa 11,300 km.
#7 Mpaka mwaka 2011 iliaminika kuwa mlima mrefu katika mfumo wa jua ni mlima Olympus mons katika sayari ya Mars wenye urefu wa 21.9 km.
#8 Mlima Rheasilvia unaopatikana katika Vesta Astroid una urefu wa 23km ndiyo mlima mrefu zaidi mpaka sasa katika mfumo wa jua (solar system)
#9 Pamoja na kutokea kwa mmomonyoko wa udongo (soil erosion) unaosababisha na mvua na upepo milima imekuwa ikipungua kwa kiasi kidogo sana, kuna wanasayansi wanaoamini katika kinachoitwa "Isostacy theory"

Source: Kalamu yangu

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends