Juma Kaseja, tajiri anayekipiga na Mbeya City FC (Sehemu ya Pili)

on Wednesday, May 4, 2016 - No comments:


Na: Mwanakalamu

Sehemu iliyopita ya simulizi hii tuliishia pale Kaseja mdogo kutoka katika kijiji hichi kilicho kando kando ya ziwa Nyasa upande wa Tanzania aliyekuja na kipande cha gazeti moja la michezo nchini Malawi chenye picha ya Juma Kaseja,tuendelee na simulizi hii ya kusisimua.
Nilimtazama yule mtoto kwa huruma kwani nilihisi  redio ni kitu pekee kilichomfanya akawa na mahaba ya dhati kwa mwanamichezo huyu nguli nchini.Nilimhurumia pale nilipofikiri kama Maji maji itashuka daraja , nafasi yake ya kumwona Juma Kaseja ingekuwa ndogo sana katika maisha yake.Pia nilifikiria kama Juma Kaseja baada ya kumaliza mkataba wake pale Mbeya City ataenda timu gani? 
Atarudi Dar es Salaam? 
Ataongeza Mkataba Mbeya City?
Atakuwa wapi?
Nikamshukuru yule mtoto  kwa kifungua kinywa chake alichonipa na kumuuliza kama ataweza kunipelekea ziwani ili nami nikalishangae tena luile ziwa nililokuwa nimekaa juu yake kwa siku kadhaa nikiwa na hofu kuu.
Akiwa na furaha alikubali kunipeleka, kwa kuwa ilikuwa Jumamosi watoto wengi walikuwa mitaani wakienda na kurudi kutoka ziwani na ndoo kichwani, samaki mkononi.
''Mbona kila anayetoka ziwani anarudi na samaki?''Namuuliza rafiki yangu mpya nikiachana kabisa na mwenyeji wangu ambaye alikuwa shuleni.
''Wamewanunua wengine wanapewa tuu, kama yule pale kapewa''Anaongea akimwonesha mama mmoja aliyekuwa na rundo la samaki wabichi mikononi.
''Umejuaje?''
''Nimejua kwa kuwa samaki wale si wa kununua wale unapewa tuu''
''Kwa hiyo hata sie tutapewa?''
''Ndiyo tukikuta wanatoka kuvua tutapewa na wewe mgeni ndo utajaziwa''
'Ila naona aibu kuomba''Naongea nikimtazama usoni yule rafiki.
''Usijali wakiniona nipo na wewe halafu nikaenda utaona maajabu ya kaseja kufunga magoli''Alijigamba akimalizia na kicheko.
''Kaseja si golikipa atafungaje magoli?''Namuuliza kwa kumtega.
''Aliwafunga Yanga kwa penati kipindi cha marehemu Mafisango siku ile ya tano bila, pia akiwa Yanga aliwahi kufunga magoli mawili kama sikosei pia alitoa pasi ya goli siku ile Okwi alipofunga dhidi ya waarabu kwenye ule usiku wa maajabu tulipotia kitumbua mchanga''Ananikumbusha mengi juu ya umahiri wa Juma Kaseja na kuniacha mdomo wazi.
''Lakini pia alikosa penati kule Sudan''Namkumbusha.
''Nakumbuka achana na kukosa penati yule jamaa anadaka sana penati , kama nifanyavyo mie''Ananikumbusha hilo rafiki yangu huyo.
''Naaam huyo ndiye Juma Kaseja'' Naongea wakati huo tulikuwa tumeshafika ziwani tunaamua kukaa kwenye mchanga ufukweni.
Tukutane kesho katika kisa hiki cha kweli kumuhusu Tanzania one aliyebaki kwenye soka.

Tagged as: ,
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends