Moyo mpweke (Nani nimuweke moyoni)

on Friday, May 13, 2016 - No comments:


SHAIRI
Moyo wangu ni mpweke,kupendwa ninatamani,
Ila nimepigwa teke,hauna tena thamani,
Upo wapi njo udeke,usinombe samahani,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Asiwe kiruka njia,leo wangu kesho sina,
Aiweke yake nia,nami nimpende sana,
Akiona ninalia,anitake kupambana,
Nani nimweke moyoni, awe radhi myaka yote.

Tangu siku ninaachwa,na muhibu tunda langu,
Kutwa mi naachwa,silijui kosa langu,
Nilienda kichwakichwa,nitulize moyo wangu,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Si utani kweli tupu,moyo wangu u mpweke,
Siipendi tena supu,wala mahindi mateke,
Siyajui magrupu,nimeshakuwa mpweke,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Kila moja nina wangu,hakuna aliye singo,
Nikienda wanguwangu,naweza vunjwa mgongo,
Njia yangu sa ni chungu,nusu niivunje shingo,
Nani nimweke moyoni,awe nami myaka yote.

Nalala mimacho wazi,nausubiri ujumbe,
Mlango naacha wazi,mawazo we siombe,
Nikipigia wazazi,naiwaza hata pombe,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Hayupo kapata bwana,nabaki nayumbayumba,
Atamba bonge la bwana,tena aitwa mchumba,
Huyu naye ana bwana,wala siyo ombaomba,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Simu sasa nakatiwa,dakika zinabakia,
Eti mori wasumbuwa,mume ananipigia,
Pia kaa ukijuwa,mjanja katangulia,
Nani nimweke moyoni,awe radhi myaka yote.

Machozi yanizuia,kuandika ninalia,
Kama upo wasikia,njoo nitakupokea,
Cha msingi zingatia,napenda upende pia,
Niandikie nikujuwe,ukiona waweza penda.

Tagged as: ,
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends