Taarifa kuhusiana na mchezaji kutoka Cameroon Patrick Ekeng aliyepoteza maisha uwanjani

on Saturday, May 7, 2016 - No comments:

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya soka barani Ulaya huenda utakuwa umekutana na taarifa za kusikitisha kwa taifa la Cameroon, usiku wa May 6 2016 Cameroon na Afrika  kwa ujumla ilipata taarifa za kushtusha, baada ya kupokea taarifa za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon aliyekuwa anaichezea Dinamo Bucuresti Patrick Ekeng.

ryder-matos-y-ekeng-presentacion-8
Ekeng enzi za uhai wake
Ekeng amefariki baada ya kuanguka uwanja dakika ya 70 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Romania uliokuwa unahusisha klabu yake ya Dinamo Bucuresti  dhidi ya Viitorul, mchezo ambao ulikuwa unarushwa live kwenye TV, tukio la Ekeng kuanguka limetokea wakati akiwa kasimama peke yake bila ya mpira.
mbia
Mbia alipost picha waliyopiga pamoja wakiwa timu ya taifa ya Cameroon
Taarifa za kifo cha Ekeng ambaye zilithibitishwa masaa mawili baada ya kufikishwa hospitali, zinakuja baada ya miaka 13 toka Cameroon impoteze kiungo wake Marc-Vivien Foe kwa stahili kama hiyo, tukio ambalo lilitokea June 26 2003 wakati wa michuano ya Kombe la mabara iliyokuwa inafanyika Ufaransa na mchezo ulikuwa dhidi ya Colombia.
mbiaa
Beki wa Arsenal Bellerin na mshambuliaji wa Man United Anthony Martial ni miongoni mwa mastaa walioguswa na kifo cha Ekeng
Ekeng alizaliwa March 26 1990 na amefariki akiwa na umri wa miaka 26 baada ya kuanguka uwanjani, Ekeng ndio alikuwa kaanza kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon ya wakubwa, muda mchache baada ya taarifa za kifo chake kuthibitika, mastaa wa soka walianza kupost na kuonesha huzuni kwa taarifa hizo.

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends