Usimhukumu mtu bila kumsikiliza, mpe nafasi kwanza.

on Monday, May 30, 2016 - No comments:


Kuna mwalimu wa shule moja ya sekondari alikuwa amezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji. Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni.

Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni mapema sana kabla ya mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita yule mwanafunzi na kumsifia sana mbele ya darasa. "Rose, simama. Darasa, Mpigieni makofi "Rose" kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia enhe"

Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka huyo "Rose". Baada ya wanafunzi kumcheka na kumfanyia dhihaka Rose alimwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo. Mwalimu akamruhusu.

Kwa sauti ya upole akasema, "Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa. Nimelelewa na mama yangu tu. Simjui ndugu yeyote. Mama yangu alipokumbwa na maradhi alipelekwa hospitalini lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na dawa za kutuliza maumivu tu. Kwa sababu hatuna pesa, hakuweza kupelekwa popote kwa vipimo zaidi." Rose alifuta machozi yaliyoanza kutiririka mashavuni, akamtizama Mwalimu wake kusha akaendelea; "Hivyo kwa kipindi chote nilichokua namuuguza mama, nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba, kuchota maji, kumsafisha mama yangu, kumwandalia chakula chake kabla ya kuja shuleni." Rose alinyamaza kidogo kisha akaendelea; "Lakini leo nimewahi kwa sababu mama yangu alifariki wiki lililopita. Kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndo maana leo nimewahi shuleni." Baada ya hapo Rose hakuweza kuongea tena. Taratibu akakaa kitini huku akilia kwa kwikwi. Darasa zima liligeuka mahala pa msiba na simanzi kuu.

FUNZO: Usimhukumu mtu bila kumpa nafasi ya kumsikiliza.!

Tagged as: ,
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends