Idadi ya wanafunzi waliokidhi vigezo (CHuo kikuu Dodoma)yawa chini ya asilimia 5

on Tuesday, July 19, 2016 - No comments:

WANACHUO 382 kati ya 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamerudishwa chuoni baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa.
Aidha wanafunzi wengine 52 waliopata daraja la nne kinyume na matakwa ya programu hiyo hawataendelea na masomo kwa kuwa hawana sifa hiyo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanafunzi hao ambao walirejeshwa nyumbani na serikali Mei 28, mwaka huu. Profesa Ndalichako alisema baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi hao chuoni kuchukuliwa, serikali ilifanya uchambuzi kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao.
Alisema sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu na alama mbili au zaidi za ufaulu katika masomo ya Sayansi na Hisabati. Alisema wanafunzi hao waliorudishwa UDOM wana ufaulu wa daraja la kwanza hadi la pili, ambao pia wamefaulu masomo mawili ya sayansi kwa kiwango cha C – A. “Wanafunzi hao 382, wa mwaka wa kwanza ni 134 na wa mwaka wa pili ni 248. Hao ndio pekee watakaorudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma ili wakamalizie mafunzo yao katika chuo hicho,” alisema.
Profesa Ndalichako alisema wanafunzi wengine 4,586 wa mwaka wa kwanza wa programu hiyo maalumu ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu, watahamishiwa katika vyuo vya ualimu vya Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo yao.
Vile vile wanafunzi 1,337 wa mwaka wa pili, watahamishiwa kwenye vyuo vya ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao. “Wanafunzi 290 waliokuwa wamedahiliwa kusoma programu maalumu ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana sifa stahiki wanashauriwa kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizonazo kwenye chuo chochote wanachotaka wao,” alisema Waziri huyo.

Tagged as: ,
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends