Tujifunze jinsi ya kujiokoa ikitokea dharura ya moto ndani

on Friday, August 12, 2016 - No comments:

  1. Kitu cha muhimu ni kutoka nje salama haraka iwezekanavyo (as soon as possible).
  2. Hakikisha (ensure) kila siku mlango wa dharura (emergency exit) ya nyumba ni umekaa kwa urahisi iwezekanvyo (as simple as possible). Kila mtu ajue funguo za milango ya kutokea zinapowekwa, Have an ermegence exit whenever possible.
  3. Fahamu kwamba ktk matukio mengi ya moto (in most cases) kinachoua ni moshi kabla ya moto, hivyo ukiona dalili ya moshi hakikisha unakuwa na kitambaa kibichi cha kujifunika puani na mdomoni, na kama moshi umeanza kuingia ulipo tambaa chini (crawl down) sababu hewa ya uhai (oxygen) ina uzito (density) kubwa kuliko hewa ya kifo (carbon monoxide) hivyo inakuwa imekandamizwa chini sentimita chache kutoka kwenye sakafu (few centimeters from the floor). Hivyo tembea kwa kutambaa.
  4. Hakikisha unawajulisha watu wote (Ensure you alert everybody) kama wamelala ili waweze kutoka nje haraka.
  5. Achana na fikra ya kuokoa vitu, ktk hatua hii cha muhimu ni kuokoa uhai kwanza.
  6. Kumbuka, muda ni kitu cha msingi, fanya haraka iwezekanavyo (quick as possible) katika kujiokoa na kuokoa wengine.
  7. Ni muhimu nyumba zetu kuziwekea kiashiria moshi (smoke detectors) na pia kizima moto (fire extinguishers). Kugundua haraka (early detection) ya moto ni muhimu sana ili kuweza kuudhibiti kirahisi. Smoke detector ni mashine ya elektroniki ambayo inagundua moshi ktk hatua ya mwanzo kabisa na itapiga kelele (alarm) kwa sauti ya juu, itakusaidia kuamka hata kama upo usingizini na kuweza kujiokoa na kuokoa wengine na kuuzima moto kabla hujashika kasi.
Na. Haji Mnasi (DED-Ileje District)

Tagged as:
Unknown About Unknown

“You have no idea how much the last few days have meant to me," I began. "Meeting you has been the best thing that's ever happened to me.” Get the latest entertainment updates from Best Hope Media or call +255 655 987 588

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

Related posts

0 comments:

Like, share and send to friends